fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Afya Tanzania

Uvaaji wa miwani ya urembo ni hatari kwa afya ya macho yetu

Uvaaji wa miwani ya urembo ni hatari kwa afya ya macho yetu

Spread the love

Katika dunia ya leo sio kitu cha ajabu kumuona mtu (wanaume/wanawake) akiwa amevaa miwani ambayo hamsaidii kitu chochote ila tu kwa ajili ya kuwa na muonekano wa kuvutia kwenye uso wake bila ya kujua kuwa miwani ya urembo ni hatari kwa afya ya macho yetu.

Utandawazi ambao unachagizwa na ukuaji wa teknolojia kwa makampuni mbalimbali kutengeneza bidhaa mathalani miwani ambazo hazitengenezwi kuja kusaidia kutibu/kuimarisha afya ya macho imekuwa ni jambo ambalolimesbababisha idadi ya watu wanaougua magonjwa ya macho nchini Tanzania. Kwa mujubu wa Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema hivi sasa kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa macho kutokana na uvaaji wa miwani isiyokuwa ya tiba na matumizi ya dawa ya macho kiholela (bila ushari wa daktari).

Katika kila wagonjwa 100, wanne kati yao wanabainika kuwa na ugonjwa wa macho; mtu mmoja anakuwa na tatizo la upofu huku watatu wanapatikana na tatizo la uwoni hafifu. Idadi hiyo inaweza kuongezeka iwapo watu hawatafuata ushauri wa daktari~Mhe. Ummy Mwalimu (Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wzee na Watoto nchini Tanzania).

miwani ya urembo

Moja ya miwani isiyokuwa ya tiba inayotengenzwa na Snapchat Inc.

Kwanini watu wanaugua ugonjwa wa macho?

Mbali na sababu za awali, kuvaa miwani ya urembo/unywaji wa dawa za macho bila ushauri wa daktari ni ulaji wa mboga za majani na matunda ambao hauridhishi vitu ambavyo vinazalisha vitamini A muhimu sana kwa afya ya macho.

Tunashauri kwenda kuangalia afya ya macho yetu kila mwaka na kuacha kutumia miwani ambazo mwisho wa siku zitatusababishia kupoteza uwoni au kupata matatizo ya macho.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania