fbpx
Gari, Intaneti, Teknolojia

Gari la Mitsubishi Outlander linaweza kudukuliwa kwa njia ya WiFi

mitsubishi-outlander-linaweza-dukuliwa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Gari aina ya Mitsubishi Outlander linaweza kuzimwa na mdukuzi kupitia teknolojia ya wi-fi iliyo kwenye gari hilo. Timu ya watafiti kutoka Pen Test Partners” waliweza kudukua wi-fi ya gari aina ya “Mitsubishi Outlander Hybrid SUV”.

Katika udukuzi huo uliwezesha wahusika na kuwawezesha kufanya chochote kile katika gari hilo na hata kuweza kuzima king’ora cha gari hilo. Mwanya huo unamaanisha kwamba wezi wanaweza kuingia na kutumia tatizo hilo la usalama wa gari hilo (Mitsubishi) kupata muda wa kuvunja, kuingia na kuliiba gari hilo.

Mdukuzi anaweza kuzima mfumo wa alarm za kiusalama wa gari hilo, pia kuingilia mfumo wake wa taarifa za hali ya hewa na hata kuwa na uwezo wa kuzima na kuwasha taa za gari hilo.

INAYOHUSIANA  Helikopta inayotengenezwa Tanzania kuruka 2018
Mitstubish
 Mitsubishi Outlander Hybrid

Iliwachukua siku nne kwa Bw. Ken na timu yake kuweza kudukua gari hilo. Mitsubishi imewataka watumizi wa magari hayo kuzima mtandao wa gari hilo huku ikiendelea kuchunguza tatizo hilo na mfumo wa gari hilo.

Tatizo kubwa likiwa ni Mitsubishi’s app ambayo inatumia wi-fi na kumuwezesha mmiliki wa gari hilo kuweza kuweka ni muda gani gari hilo litaweza kuchaji, kuweza kuzima taa za gari lakini pia kuweza kuzima king’ora (alarm) cha gari hilo. Ili kuweza kutumia wi-fi ya gari hilo inabidi mtumiaji awe na SSID na neno siri(password) lakini hata hivyo Bw. Ken alisema havijitoshelezi kuweza kulinda gari hilo kutodukuliwa.

Mitstubish1
Mitsubishi Outlander Hybrid

Mtaalam wa masuala ya kiusalama Bw. Ken Munro anasema kuwa uchunguzi ulianza wakati alipokuwa akingojea kuchukua watoto wake kutoka shule na kubaini kudukuliwa wa mtandao wa gari hilo katika orodha ya simu yake na kuongeza kuwa kama yeye angekuwa mwizi cha kwanza kufanya kwa sababu gari hiyo inatumia wi-fi basi angeitafuta wi-fi ya gari hilo kisha kulitafuta gari lilipo na kutuma code ya kuzima king’ora cha gari hilo na baada ya hapo angevunja kioo na kufungua mlango wa gari kuingia ndani ya gari. Mwisho wa siku angelishakuwa ameiba gari hilo.

INAYOHUSIANA  Facebook Kubadilisha Sera ya Kutumia Majina Halisi
Muonekano wa Mitsubishi Outlander SUV
Muonekano wa Mitsubishi Outlander SUV

Hata hivyo timu hiyo ilivyowasililiana na Mitsubishi walisema wao kuweza kuduakua king’ora cha gari hilo sio kitu cha kushangaza kwa sababu siku hizi kudukuliwa kwa vitu imekuwa jambo la kawaida kwahiyo haitaweza kuboresha ulinzi katika gari hilo.

Wao kama kampuni watakachokifanya ni kuboresha ulinzi katika gari hilo na watajionea wenyewe litakapokuwa likizinduliwa mwaka huu nchini Marekani. Gari hili linauzwa kwa bei ya zaidi ya Tsh Milioni 90 za Kitanzania.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|