fbpx
Huawei, Sayansi, Teknolojia

Mishahara Minono Huawei: Huawei inavutia wafanyakazi kwa ahadi nono

mishahara-minono-huawei
Sambaza

Tangazo la kazi na ahadi ya mishahara minono limetolewa na Huawei. Kama upo vizuri kwenye hesabu, sayansi na teknolojia basi Huawei imetangaza italipa mshahara wa hadi mara tano ukilinganisha na mishahara ya watu wengine wenye kazi kama yako.

Kampuni ya Huawei inajaribu kuvutia mabingwa na wabobezi wa maeneo mbalimbali ya sayansi na teknolojia uli kuweza kukua kwa haraka kupitia kubuni na kutengeneza teknolojia zake za kipekee.

INAYOHUSIANA  Ndege Ndogo Yakamatwa Ikiwa Inasafirisha Bangi Gerezani

Kwa sasa katika bidhaa za Huawei kama simu kuna asilimia kubwa ya teknolojia/vipuli vya ndani ambavyo vinahusika kununua au kulipa leseni ya utumiaji kwa makampuni mengine – mengi yakiwa ya Marekani.

Huawei imeamua kuwekeza zaidi katika utafiti na ubunifu wa teknolojia zake ili iwe huru na kuepuka matatizo kama wanayopitia kwa sasa kama madhara ya ugomvi wa kibiashara kati ya serikali ya Marekani na Uchina.

INAYOHUSIANA  StoreDotFlashBattery: Betri inayojaa chaji chini ya dakika moja! #Teknolojia

Kwa sasa mshahara wa juu kabisa kwa wafanyakazi wapya vijana katika kampuni hiyo unaweza kufika hadi milioni 600 – 700 za Kitanzania kwa mwaka.

Tangazo la Huawei la ajira hizo ni hili hapa:

mishahara minono Huawei
Kazi na Mishahara Minono Huawei: Kwa kulipa vizuri Huawei wanaamini wataweza kuvutia watu bora zaidi
Chanzo: TheStar
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |