fbpx

Microsoft: Serikali inachoifanyia Huawei si sawa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Serikali inachoifanyia Huawei si sawa, hayo ni maneno ya mmoja wa kiongozi wa juu kabisa ndani ya kampuni ya Microsoft .

Rais wa kampuni hiyo na ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa kampuni hiyo bwana Brad Smith alisema hayo alipokuwa katika mahojiano na chombo cha habari cha Bloomberg. Bwana Brad amesema jambo ambalo serikali hiyo inafanya dhidi ya Huawei ni jambo ambalo halina sifa ya misingi ya taifa la Marekani.

Brad Smith rais wa Microsoft

Brad Smith, Rais wa Microsoft: Serikali inachoifanyia Huawei si sawa

Bwana Brad amesema serikali ya nchi hiyo imeshindwa kutumia misingi ya kimahakama ya kushtaki na kuleta mbele ushahidi dhidi ya shutuma zake dhidi ya Huawei na pia kuipa kampuni hiyo nafasi ya kujitetea.

Amesema kwa sasa kila wakizungumza na serikali ya nchi hiyo juu ya zuio linalowahusu wao pia la kufanya biashara na Huawei jibu wanalopata ni ‘mngejua tunachojua, mngekubaliana na sisi’ ambapo Microsoft na wadau wengine wamekuwa wakitoa majibu ya ‘basi tuonesheni hicho mnachojua ili nasi tuwe na uelewa mzuri’ lakini hadi sasa serikali na vyombo vya usalama havijawapa ushahidi wowote wa ubaya wa Huawei.

Marekani wazidi kuibana Huawei

Vita hii inaonekana kuhusisha sana teknolojia ya 5G na uwezekano mkubwa wa ukuaji wa kampuni ya HUAWEI kwenye sekta hii

Suala la Huawei kuwa katika nafasi ya mbele zaidi katika teknolojia ya 5G ni mwiba mkubwa kwa vyombo vya usalama vya mataifa ya magharibi.

INAYOHUSIANA  Amazon kuleta Headphone ambazo ukiitwa jina zinazima

Teknolojia ya 5G inategemewa kuwa muhimu sana katika sekta zote muhimu za uchumi na hivyo kumaanisha kampuni ya Huawei kama itauza vifaa na kufunga mitambo kwenye mataifa mengi basi itakuwa ni moja ya makampuni yenye nguvu sana katika sekta nzima ya mawasiliano na usalama wa kidigitali.

Hofu kubwa kwa Marekani ni kwamba jambo hili linaweza kutumiwa kwa ukaribu na serikali ya China katika kudukua data mbalimbali – za kiuchumi, kiusalama na ata za kisiasa za mataifa ya magharibi kama yatatumia vifaa vya 5G kutoka Huawei.

INAYOHUSIANA  Kwa Kushangaza Kabisa, Pengine Hii Ndio Simu Ya Mwisho Ya Microsoft Inayotumia Jina La Nokia!

Ubaya ni kwamba hadi sasa Marekani hawajaweka wazi uthibitisho wa madai yao kuonesha Huawei inashirikiana na serikali ya China kwenye jambo lolote kama hilo. Kampuni hiyo imekana shutuma hizo mara zote.

Vyanzo: Yahoo na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.