fbpx

Microsoft kwenye iPhone: Word, Excel, na Powerpoint kuwa kwenye app moja

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Microsoft wapo njiani kuja na mabadiliko ya apps za huduma zake kwenye simu za iPhone. Wanatengeneza app moja itakayotoa huduma za Excel, Word na Powerpoint, tofauti na sasa ambapo ni apps tofauti.

microsoft kwenye iphone

Microsoft kwenye iPhone: Kwa sasa huduma za Word, Excel na Powerpoint zinapatikana kwenye app tofauti

Jambo kama hili tayari limefanyika kwa ushirikiano na Samsung, ambapo toleo la app ya Microsoft Office Mobile linapatikana katika soko la apps la Samsung – Galaxy App Store. Ni app moja isiyo nzito inayoweza kufungua mafaili ya Word, Excel na PowerPoint.

INAYOHUSIANA  Fahamu Samsung Galaxy S6 na S6 Edge

Katika toleo la app hii kwa ajili ya iPhone timu ya Microsoft ya nchini India ndio inalifanyia kazi jambo hili na toleo la app linategemewa kufikia mwaka 2020.

Kwa watumiaji wa Android wanaotumia simu za Samsung tayari wanaweza kupakua app hiyo kupitia soko la apps la Samsung kwenye app ya Galaxy App Store. Kwa watumiaji wengine wa Android inategemewa toleo linaweza likaanza kupatikana kwenye Google PlayStore hapo baadae.

Microsoft office app microsoft kwenye iphone

Kwenye soko la apps la Samsung, Galaxy App Store.

Ushirikiane wake na Samsung katika utengenezaji wa app hii unaweza kuwa na maana itachukua muda hadi app hiyo kuanza kupatikana kwa watumiaji wa simu zingine.

INAYOHUSIANA  Apple wataka simu zao ziwe na uwezo wa kuwa laptop kamili! #Teknolojia

Tuambie una mtazamo gani juu ya toleo hili la app moja kwa ajili ya mafaili ya Word, Excel na Powerpoint? Soma zaidi habari za Microsoft -> Teknokona/Microsoft

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.