Teknolojia ya simu ambazo zinakunjika inaonekana kushika kasi kwa maana ya kwamba kurudi tena machoni pa watu lakini ikiwa katika mtndo ulio bora zaidi kuliko ule wa zamani kwani Microsoft nao watatoa rununu ya aina hiyo.
Kwa miezi kadhaa sasa Microsoft imekuwa ikiwa mafichoni kutengenza simu janja ambayo itakuwa na uwezo wa kukunjika kama ambavyo makampuni mengine nayo yakiwa tayari wameshazindua.
Microsoft wao kwa mujibu wa taarifa za kuaminika imebainika simu hiyo itatoka mwaka 2019 lakini pia tayari picha za bidhaa yenyewe ilivyo zimeshaonekana na kuongeza hamasa kubwa kwa wapenzi wa vitu kutoka kampuni husika.
Simu yenyewe inaitwa Microsoft Andromeda na inaaminika kabisa itatumia Snapdragon 850 kama kipuri mama huku Windows 10 ukiwa ndio mfumo endeshi kwenye simu hiyo.
Mbali na ujio wa simu hiyo pia Microsoft wanategemewa kutoa Xbox One toleo jipya, vipakatalishi (Microsoft Surface) ikiwa na vipuri vya AMD, Surface Studio toleo jingine na tabiti itakayoshindana na iPad Pro 12.9.
Vyanzo: NDTV, GSMArena, The Indian Express