Kampuni ya Microsoft chini ya kitengo chake cha michezo kijulikanacho kama Xbox kimetangaza kuwa kitainunua kampuni ya Beam.
Beam nayo yenyewe inajihusisha na maswala ya magemu na hata yale ya ‘Live Streaming’ yaani mtu au watu wanaweza kucheza michezo hiyo moja kwa moja kwa kutumia mtandao unaowaunganisha.
Beam kama kampuni licha ya kuwa na mafanikio makubwa lakini ukweli ni kwamba inaendeshwa na kijana ambae ana umri wa miaka 18.
Kijana huyo anajulikana kama Matt Salsamendi ambae alianzisha kampuni ya Beam ambayo kwa sasa ina wafanyakazi 24.
Ununuzi wa kampuni ya Beam utaisaidia kampuni ya Microsoft katika kukuza mbinu za Xbox Live ambayo ni moja kati ya sehemu ya kijamii maarufu inayohusiana na michezo (magemu).
Kwa upande mwingine Beam imeshinda mambo kadhaa tangia ianzishwe. Ilikuwa ni mshindi katika moja ya mashindano na ikajinyakulia kitita cha dola za kimarekani elfu 50. Matt na mwenzie ambae walibuni wote Beam walitajwa kama chipukizi wanaokua kwa kasi mwezi juni 2016.
Beam tayari ina wanachama 100,000 katika jamii yao ya wanamichezo na hivyo ikijichanganya na namba uile katika Xbox Live namba itapanda zaidi hivyo mafanikio makubwa yatafikiwa.
Niandikie sehemu ya comment hapo chini nini kimekuvutia katika hii? Kumbuka jamaa bado ni mdogo sana (miaka 18) na kagundua kitu ambacho Microsoft wana mpango wa kukinunua. Ningependa kusikia kutoka kwako.