Je unategemea kununua kompyuta/laptop ya kisasa zaidi hivi karibuni? Jiandae kutumia Windows 10 tuu kwenye kompyuta hizo.
Microsoft wamesema watazuia updates (masasisho) kwa kompyuta/laptop zote za kisasa kama zinatumia matoleo ya Windows 7 au Windows 8.1. Uamuzi huu unaonesha ni kwa namna gani Microsoft wanalazimisha kompyuta zote mpya za kisasa kutumia toleo la Windows 10.
Kigezo gani kinatumika watu kushindwa kupokea updates/masasisho?
Kompyuta zitakazogundulika zinatumia chips/Prosesa za familia ya Intel 7, AMD Ryzen na Qualcomm 8996. Baadhi ya chip/prosesa za kisasa kidogo zitaendelea kupata masasisho (updates) kwa miaka kadhaa mbele.
Kwa kompyuta zenye prosesa (CPU) za miaka ya nyuma kama vile Intel 6 (Skylake) zitaendelea kupata masasisho ya Windows 7 hadi Januari 14, 2020, kama kompyuta hiyo inatumia Windows 8.1 itaendelea kupata masasisho hadi Januari 10, 2023.Ikifika kipindi hicho itakuwa ni lazima kompyuta iwe inatumia toleo la Windows 10 ili iweze kupata masasisho.