Imekuwa ni jambo la kawaida kwa makampuni yanayofanya biashara ya simu janja kuweka wazi mpango wao wa kupeleka masasisho ya programu endeshi halikadhalika yale yanayohusu kifaa kuzidi kuwa salama ambayo hutoka kila mwezi.
Kampuni ya Samsung imeweka wazi mpango wake wa kupeleka masasisho ya programu endeshi kwa miaka minnne (4) na miaka mitano (5) ya maoboresho yanayotoka kila mwezi. Simu janja ambazo zipo kwenye mpango huo ni zile ambazo zimetoka katoka miaka ya karibuni kabisa pamoja na toleo la nyuma kidogo kutoka familia ya “A” na “M”.
Samsung imeweka imeahidi kwa dhati kabisa kutoa masasisho ya programu endeshi mpaka toleo la Android 16 na kwa upande wa maboresho ya kuifanya simu janja kuwa salama ni hadi mwaka 2027 zikihusisha Samsung Galaxy S22 na tabiti za Galaxy S8.
Halikadhalika, zile simu janja zilizotoka mwaka 2021 kama familia ya Galaxy Z3 zinazokunjika/kukunjuka, Galaxy S21 na nduguze ikiwemo Galaxy S21 FE. Galaxy S20 na nduguze zitapokea masasisho mpaka Android 16. Zile zinazoweza kukunjika/kukunjuka toleo la nyuma kidogo zinabaki kwenye mpango wa mika minne (4) ya kukokea masasisho.
Samsung Galaxy Z Flip 3: Mojawapo ya simu janja ambazo zitapokea masasisho ya hadi Android 16 pamoja na yale menginyo mpaka 2027.
Jedwali la simu zote za Samsung ambazo zitapata masasisho hadi toleo la Android 16
Rununu hizi zimepangwa kulingana na familia inayotoka. Fuatana nami kuweza kuzifahamu.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.