fbpx

Miaka 25 ijayo huenda mwanadamu akatua Sayari ya Mars

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Shirika la Utafiti anga za juu la Marekani (NASA) limesema linaamini miaka 25 ijayo litaweza kupeleka binadamu katika sayari ya Mars huku likiangalia namna ya kutatua vikwazo vikubwa vya kiteknolojia na matibabu.

Mionzi mikali inayosababisha vifo kutoka anga la Cosmos, uwezekano wa kupoteza uwezo wa kuona na mifupa kutepeta ni baadhi ya changamoto ambazo wanasayansi lazima wazikabili na kuzishinda kabla ya mwanaanga yeyote kutia mguu katika Sayari Nyekundu.

Miaka 25

Kwa jinsi bajeti inayotengwa kwa ajili ya masuala ya anga itachukua miaka robo karne binadamu kuweza kufika Mars.

Kwa umbali wa wastani wa kilomita 225 milioni, sayari ya Mars inaibua matatizo ya kisayansi tena makubwa zaidi kuliko kitu chochote kilichowahi kufikiwa katika safari za mwezi kwa kutumia chombo cha Apollo.

Kwa msaada wa teknolojia ya roketi inayotumika leo, itamchukua mwanaanga hadi miezi tisa kufikia Mars.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.