fbpx
Tanzania, Teknolojia

Fahamu mfumo mpya usajili wa laini za simu

mfumo-mpya-usajili-wa-laini-za-simu
Sambaza

Serikali imesema itaanza kudhibiti umiliki holela wa laini za simu kwa kutumia njia ya usajili wa alama za vidole za mtu atakayetaka kusajili laini.

Pamekuwepo taarifa mbalimbali kuhusu suala zima la kumiliki simu jambo ambalo limeleta mkanganyiko na pengine kuna watu bado hawajaelewa vizuri au kutoelewa kabisa kuhusu mpango mpya wa kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole.

INAYOHUSIANA  Sony yazindua simu janja yenye kamera bora duniani

Hivyo basi serikali inashirikiana na NIDA, Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Mawakala wa Vizazi na Vifo (RITA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa maana ya kwamba taarifa ambazo mtu ataziainisha siku anapokwenda kusajili laini yake zitakuwa ni taarifa sawasawa zilizopo NIDA, NEC, TCRA, n.k.

Sasa mkanganyiko ulipotokea ni pale ambapo mtu atahitaji kuwa na laini zaidi ya moja lakini ni wazi kwamba hakuna kitu chochote cha ajabu na suala zima litakuwa hivi:

Utakapoenda kwenye kituo cha kusajili laini nyingine itakubidi ujaze fomu na kama taarifa hizo zikiwa ni tofauti na zile ulizosajilia kwa njia ya alama ya kidole ndio hapo utakapoleta walakini na kutaka kujua kwanini taarifa ulizojaza kwenye fomu ni tofauti na za kwenye kanzi data.

laini za simu
Usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole unatazamiwa kupambana na uhalifu.

Mpango huo kwa sasa upo katika hatua za majaribio na mpka sasa vituo mbalimbali vianzishwa kuweza kusajili laini za simu kwa kutumia alama za vidole; kituo kimojawapo kipo Mlimani City.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.