Mapema asubuhi ya tarehe 15 Aprili mwaka 1921, meli kubwa ya abiria ya Titanic ambayo iliwahi kusifiwa kuwa maajabu kwenye historia ya viwanda duniani iligonga barafu na kuzama katika bahari ya Atlantiki, na kusababisha vifo wa watu zaidi ya 1500.
Meli hiyo iliyotajwa kuwa kubwa zaidi kubeba abiria kipindi chake, mabaki ya meli hiyo yaligunduliwa chini ya bahari mwaka 1985.

Hivi karibuni wanasayansi wamesema vijidudu vinaozesha mabaki ya meli hiyo siku hadi siku, na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030, meli hii itatoweka kabisa.
Kabla ya hapo watu waligundua kuwa meli hiyo inaoza. Kikundi cha wachunguzi wa mabaki ya Titanic kilifanya uchunguzi kwa mara zaidi ya 30 kuanzia mwaka 1987 hadi miaka ya 90 karne iliyopita, wachunguzi wamerekodi kubomoka kwa paa la vyumba vya meli, kuharibika kwa sitaha na kutoweka kwa milingoti na ulingo.
Mtaalamu wa taasisi ya bahari ya Woods Hole Bw. Bill Lange alisema watu wana maoni tofauti kuhusu muda wa kuwepo kwa mabaki hayo, baadhi ya watu wanasema kichwa cha meli hiyo kitabomoka ndani ya mwaka mmoja hadi miwili, na wengine wanasema kitadumu kwa miaka mamia kadhaa.
Soma pia – Antonov An – 225 Ifahamu ndege Kubwa Zaidi Duniani!