Tumia kompyuta yako kama mtaalam/mzoefu, hii itakusaidia katika kumaliza kazi katika muda mchache. Ulishawahi kuona wale wanadokoa herufi moja moja? (ha!). Sasa utatumia vipi vizuri muda wako kama uko taratibu na hujui aina mbalimbali ya maujanja na njia za mkato ukiwa mtandaoni/intaneti? Lazima upoteze muda sio?
Nina uhakika kila mtu anapenda njia za mkato na mbinu mbalimbali wakati anapokua anatumia kompyuta yake. Sasa basi zifuatazo ndio njia na mbinu mbalimbali unazoweza tumia ukiwa katika mtandao kwa kompyuta yako.
1. NJIA YA MKATO KWENDA KWENYE WEBSITE
Haina haja ya kuandika sana ili upate kuingia katika mtandao unayoipenda. Kiurahisi andika jina la mtandao unaotaka kuingia bila kuweka ‘www.’ mwanzoni wala ‘.com’ mwiahoni kisha bonyeza CTRL+Enter itakupeleka kwenye tovuti hiyo, Mfano unataka kuingia na kusoma makala za www.teknokona.com basi andika Teknokona kisha bonyeza CTRL+Enter kwa mkupuo, mambo yatajipa
2. HIFADHI UKURASA KAMA PDF
Unaweza hifadhi ukurasa unaouhitaji kama PDF lakini hii inatengemea na ‘Browser’ unayoitumia. Ukitumia Google Chrome unaweza ifanya ukurasa kama PDF. Nenda kwenye ukurasa unaoutaka kisha bofya CTRL+P kama unatumia Windows na Cmd+P kama watumia MAC
3. PATA TENA UKURASA ULIOFUNGA/FUTA
Hili linavutia, unaweza pata ukurasa uliofunga kwa bahati mbaya. Kufanya hivyo bonyeza Ctrl + Shift + T ili kuupata tena. Vipi kama ulifunga kurasa mbili tofauti kwa bahati mbaya au hata tatu? basi bonyeza Ctrl + Shift + T mara mbili ili kupata kurasa ya pili na mara tatu kupata kurasa ya tatu na kuendelea.
4. ONYESHA URL KATIKA BROWSER
Unaweza ukaonesha (Highlight) URL katika browser kwa kubofya CTRL + L. na kisha utaamua ufanye nini mfano ukiamua kuinakili hiyo URL utabofya CTRL + C
5. NJIA RAHISI YA KUFUNGUA TASK MANAGER
Imezoeleka kufungua Task Manager kwa kutumia njia hii CTRL+ALT+DEL lakini njia hii si nzuri kwa sababu haikupeleki kwenye Task Manager moja kwa moja, inakupeleka katika menu/mchaguo fulani hivi ndani ya huo mchaguo ndio unaweza chagua Task Manager. Kwa nini upitie yote hayo? Bonyeza CTRL+SHIFT+ESC kuifungua Task Manager moja kwa moja.
6. KUUKUZA UKURASA NJE NA NDANI
Ndio unaweza kuukuza ukurasa nje au ndani (zoom in and Out). Kama haujaridhishwa na ukubwa wa muonekano wa ukurasa wako unaweza kuubadilisha, unaweza kuukuza muenekano huo au kuufanya uwe muonekano mdogo inategemea na wewe unataka nini. Ili kufanya hivyo inakubidi ubofye CTRL+ au CTRL- kisha ukubwa wa ukurasa utabadilika
7. NJIA YA MKATO KWA UKURASA MPYA
Haina haja ya kutumia nguvu njingi kufungua anuani/Link katika ukurasa unaofuata. unaweza fanya hivyo kwa urahisi tuu sogeza kipanya(mouse) yako juu ya LINKI husika kisha bonyeza CTRL na Left. Bofya hapo link itafunguka katika ukurasa mwingine
8.SIMAMISHA KWA MDA VIDEO YOUTUBE
Unaweza ukawa unatumia Space Bar kushusha ukurasa chini na kusimamisha kwa muda (pause) video za Youtube. Lakini unaweza ukatenga kazi hizi mbili. Bonyeza K kusimamisha kwa mda video na bonyeza Space Bar kushuka chini katika ukurasa huo huo mmoja
9. NJIA YA MKATO KWENDA SEHEMU YA DOWNLOADS
Hii haijilishi kama unatumia Mozila Firefox au Google Chrome. Kama unatafuta mafaili ulioshusha au yale unayo shusha bonyeza CTRL + J na utapelekwa kwenye ukurasa huo
10. NJIA YA MKATO YA KUFUTA CACHE
Unaweza ukafuta cache za ‘browser’ yako kwa kubonyeza CTRL+SHFT+R kisha refresh ukurasa huo.
Kuna mbinu kibao na maujanja mengi sana juu nini unaweza fanya na browser ya kompyuta yako. Ningependa kusikia kutoka kwako lipi halipo hapa na unalifahamu…
Kusoma maujanja zaidi, bofya hapa – TeknoKona/Maujanja
No Comment! Be the first one.