fbpx

Apple Kuachana Na 3D Touch (Mbadala Wapatiakana)!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tangia uwezo wa ‘3D Touch’ kutambulishwa katika simu za iPhone 6s na zile zingine za mbele ilikua ni teknolojia ngeni katika soko la simu janja. Hivi sasa Apple wana mpango wa kuachana na teknolojia hiyo na kuja na mpya.

Uwezo wa ‘3D Touch’ utauliwa katiak simu  zote za iPhone ambazo zitatoka katika mwaka 2019 na kuendelea. Teknolojia hiyo itapata mbadala wake anaejulikana kama ‘Haptic Touch’

Haptic Touch

Haptic Touch Katika Kuwasha Tochi

‘Haptic Touch’ kwa mara ya kwanza ilitambulishwa katika toleo la (kwanza) mwaka jana la iPhone XR. Ikumbukwe kwamba hapo nyuma teknolojia ya ‘3D Touch’ ilianzishwa huku ikiwa inafanya kazi kwa kuhisi aina ya mguso katika skrini ya simu ili kutoa chaguzi mbali mbali kama ikiwa ni njia ya mkato kabisa. Mtu ulikuwa unaweza chagua cha kufanya katika App yeyote kabla hata hujaingia katika App hiyo.

Haptic Touch.

Haptic Touch Katika Settings

‘Haptic Touch’ yenyewe haingalii ni kwa nguvu kiasi gani umegusa skrini kama ilivyo ‘3D Touch’ bali yenyewe inaangalia ni kwa muda gani umegusa kioo katika sehemu (husika unayotaka).

INAYOHUSIANA  Tegemea Mambo Haya Katika Toleo La iOS 11! #MaelezoNaPicha

Kuna mambo mengine mengi ambayo yatakuwa yameboreshwa katika ‘Haptic Touch’ ambayo mwanzoni hayakuwa katika ile ya 3D. Ili kuendelea kuyajua endelea kutfuatilia mtandao wako pendwa wa TeknoKona ili kuendelea kuhabarika

Kwa Habari Za Teknolojia Na Sayansi, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.