fbpx
Sayansi

Mayai yanayotibu ugonjwa wa saratani

mayai-yanayotibu-ugonjwa-wa-saratani
Sambaza

Wanasayansi nchini Scotland wamefanikiwa kukuza kuku wenye uwezo wa kutaga mayai yatayokuwa na dawa ya kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili na kutibu ugonjwa wa saratani.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya taarifa, Dkt. Lissa Herron na timu yake kutoka chuo cha teknolojia cha Roslin cha mjini Edinburg nchini Scotland, wamefanikiwa kuchanganya kinasaba cha binadamu na sehemu fulani ya kinasaba cha kuku inayohusika na kutengeneza ute mweupe wa yai kupata protini.

ugonjwa wa saratani
Mchakato huo hautaathiri afya ya kuku kwa aina yoyote ile. Dozi moja ya dawa hiyo itakuwa sawa na mayai matatu yaliyotagwa na kuku hao.

Mayai hayo yatakayozalishwa kutoka kuku hao yatakuwa na uwezo wa kuimarisha mfumo wa ulinzi wa binadamu na kutibu magonjwa kama saratani. Utengenezaji wa dawa kwa njia hii utashusha gharama ya kutengeneza dawa hizo hadi mara 100 ukilinganisha na uzalishaji wa dawa za ugonjwa wa saratani kutoka viwandani.

INAYOHUSIANA  Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!

Kwa mujibu wa watafiti hao ili mayai hayo yaweze kutumika kwa tiba ya binadamu inabidi ipatikane ruhusa ya kisheria; ruhusa hiyo ya kisheria inaweza kuchukua kati ya miaka 10 hadi 20 kutolewa.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.