Miaka 10-15 nyuma kabla ya ujio wa WhatsApp, Telegram, Skype ilikuwa maarufu sana kutokana na kuwezesha mawasiliano kwa njia ya picha jongegu na hata maandishi vyote vikiwezekana kufanyika kwa wakati mmoja lakini miaka ikapita na washindani wakaja na kuifanya kupoteza umaarufu wake.
Ingawa washindani wapo na wanaboresha bidhaa zao kila mara Microsoft nao hawajaiacha nyuma Skype kwakuifanya ivutie na kuendelea kupata wateja, kitu kizuri ni kwamba haijasahaulika na kuna watu mpaka leo bado wanatumia programu hiyo kufanya mawasiliano na watu sehemu yoyote duniani.
Tunafahamu vyema urahisi wa kuwasiliana na watu kwa njia ya picha ya mnato na siku hizi inawezekana kuwasiliana na watu zaidi ya wawili kwa nja ya picha jongefu kwa wati mmoja, sasa Skype imeboreshwa kwa kuwezesha kushirikisha hadi watu hamsini (50) kupitia picha mnato; kabla ya maboresho hayo ni watu ishirini na watano (25) tu ndio walikuwa nawaweza kuunganishwa kwenye mazungumzo ya pamoja.

Kabla ya maboresho hayo ilikuwa kila mtu aliyeunganishwa kwenye mawasiliano ya kundi anapata taarifa pale mtu mwingine anapoongezwa kwenye mazungumzo. Sambamba na maboresho hayo pia yule aliyeanzisha mazungumzo ya kundi anaweza akachagua ni nani anaweza akampigia yeye wakati mawasilaino ya kundi yakiendelea.
One Comment
Comments are closed.