fbpx

Mauzo ya simu janja za Huawei yaporomoka kwa 40% kutoka Mei kwenda Juni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Mauzo ya simu janja za Huawei yaporomoka kwa asilimia 40. Zuio la biashara la Marekani limeanza kuleta athari za kimapato kwa Huawei baada ya data zao kuonesha kuporomoka kwa mauzo ya simu ukilinganisha na kipindi cha mwenzi mmoja uliopita.

Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa kampuni hiyo Bwana Ren Zhengfei na baadae taarifa hiyo kukubaliwa na msemaji wa kampuni hiyo.

Mauzo ya simu janja za Huawei yaporomoka

“Mauzo ya simu janja za Huawei yaporomoka” Ren Zhengfei, Mwanzilishi na Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Huawei

Huawei wamesema asilimia hiyo ya kudondoka kwenye mauzo imesababishwa na hatua ya Marekani kuiwekea vikwazo vya kibiashara ambavyo hadi sasa vimeathiri mahusiano ya kibiashara kati ya kampuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na Google, Facebook, Intel, Microsoft na wengine wengi.

INAYOHUSIANA  Windows 10 Itapatikana 'bure' Kwa Mwaka Mmoja!

Wamesema katika soko lao la ndani – yaani nchini China bado mauzo yanaendelea vizuri bila athari yeyote. Hii inaweza isishangaze kwani simu zinazouzwa nchini humo hazina apps mbalimbali ambazo zishazoeleka nje ya China – hii ikiwa ni pamoja na Google Playstore, Gmail, Google Maps, WhatsApp, Facebook, Instagram na apps nyingine mbalimbali za mitandao ya kijamii za mataifa ya magharibi.

Huawei waliingiza sokoni simu janja milioni 206 mwaka 2018, takribani nusu ya simu hizo zikibakia nchini China na nusu yake kuuzwa mataifa mengine.

huawei china

Hali isipobadilika Huawei itawabidi wawekeze zaidi kwenye teknolojia zao za chip na pia kutokana na kukosekana kwa apps muhimu soko lako kuu linaweza kuwa ni China tuu

Bwana Ren amesema wanategemea kupunguza uzalishaji wa simu katika kipindi cha hadi miezi 24 kuweza kuelewa hali ya soko. Wanategemea mapato yatashuka kwa asilimia hadi 30 kwa mwaka huu, akiwa na mategemeo kufikia mwaka 2021 wataweza kuanza kukua tena.

INAYOHUSIANA  Motorola One nyingine kutoka Mei 15

Watafiti wengine wa masoko wanaamini mauzo hayo yanaweza yakaja kushuka kwa kati ya asilimia 40 hadi 60 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Kufahamu kwa undani sakata hili unaweza pia kusoma habari zifuatazo tulizoziandika hapa Teknokona;

INAYOHUSIANA  #Teknolojia - Upo tayari kuchaji Simu yako Mara Moja kwa Wiki?

Je una mtazamo gani juu ya vikwazo hivi? Je utaweza kununua simu ambayo inakuja bila apps za Google Playstore na zile za familia ya Facebook (WhatsApp, Messenger, Instagram)?

chanzo: Bloomberg na vyanzo vingine
Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.