fbpx

Matumizi ya Drone kwa ajili ya kuokoa maisha

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ndege zisizokuwa na rubani au maarufu kama “Drone” zimekuwa zikitumiwa kwa njia tofauti tofauti katika kufanikisha/kurahisisha jambo fulani na kuokoa muda kama njia nyingine ingetumika kufanikisha jambo hilo.

Maisha ya binadanu ni kitu ambacho hakiwezi kuwa na mbadala na kwa mara ya kwanza kampuni moja ambayo inajishughulisha na utengenezaji wa ndwge zinazoendeshwa bila ya rubani imefanikiwa kuokoa maisha ya vijana wawili waliokuwa wanakufa maji.

Vijana hao walionaswa na jicho la kamera ya ndege hiyo walikuwa mita 700 kutoka nchi kavu na mara baada ya drone hiyo kuona ilitupa kifaa cha uokozi ambacho kinafunguka mara tu baada ya kutua kwwenye maji.

Kampuni mbalimbali zimeanza kutumia ndege zisizoendeshwa na rubani katika uokozi kwa kufaniksha kunusuru maisha ya binadamu kwa haraka sana.

Ilimchukua mwongoza drone karibu dakika mbili kuweza kufika eneo la tukio na kuangusha kifaa hicho cha uokozi na kama watalaam wa masuala ya kuokoa watu kwenye maji, ingewachukua karibu dakika sita mpaka kifaa cha uokozi kiwafikie wahitaji.

Little Ripper Life Saver ndio wamiliki wa drone ambayo ilitumika katika kufanikisha kuwaokoa wahanga waliotaka kufa maji. Kampuni hiyo inaangazia zaifi kutengeneza drone ambazo zitakuwa zinawekwa vifaa vya uokozi na kuweza kusafirishwa mpaka eneo la tukio kwa urahisi na haraka.

INAYOHUSIANA  BBM300: Gari hili spesheli linafyatua matofali 300 kwa dakika! #Teknolojia

Serikali ya Kusini mwa Wales imesifia tukio hilo ambalo ni la kwanza ulimwenguni kwa drone kutumika kama msaada na kuweza kuokoa maisha ya vijana waliokuwa wanakufa maji kwa haraka (ndani ya sekunde 70).

Vyanzo: The Verge, CBS News

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|