fbpx
Android Pie, LG, simu, Teknolojia

Masasisho ya Android 9 Pie kwenye simu za LG

masasisho-ya-android-9-pie-kwenye-simu-za-lg
Sambaza

Mpaka kufikia hivi sasa simu nyingi tu zimeshaweza kuruhusiwa kushusha Androi 9 Pie lakini kitu ambacho kinawafanya wateja wa LG kwa upande w rununu kuonekana kuwa nyuma kuhusu kutumia simu zao zikiwa na toleo hilo la kenda kwa mfumo endeshi wa Android.

Ukiangazia kwa jicho la karibu kabisa simu za LG ambazo zina masasisho ya Android 9 utagundua ni chache sanana kwa uhakika kabisa ni wale wenye LG G7 na G7 ThinQ tu  ndio ambazo zimeweza kuruhusiwa kupokea sasisho hilo la programu endeshi lakini kwa mujibu wa taarifa kampuni hiyo yenye makao yake Korea Kusini itaruhusu toleo hilo kwenye rununu nne (4).

INAYOHUSIANA  Basi linalopita juu ya magari lafanyiwa majaribio China.

SImu hizo, LG V30, V30S ThinQ, V35 ThinQ na V40 ThinQ zitaweza kushusha Android Pie mwezi Juni 2019 katika hali ya kujaribu kuwafurahisha watu ambao wanamiliki simu hizo na wamekuwa wakisubiri rununu zao kuweza kuwezeshwa kupakuwa maboresho hayo kwa miezi mingi tuu.

 simu za LG
Moja ya simu za LG zitazoweza kushusha Android 9 mwezi Juni 2019.

Hakuna tarehe ambazo zimewekwa wazi kwamba ni lini simu hizo nne zitaweza kushusha sasisho la Android Pie lakini huenda mwezi Juni mambo yakaanzia nyumbani kwanza (Korea Kusini) kisha wengine wakaweza kupakua baadae kidogo.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|