fbpx

Marufuku matumizi ya Bitcoin nchini Iran

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Makamu wa rais-benki kuu, Nasır Hakimi amesema kuwa serikali ya Iran imepiga marufuku shughuli zote za matumizi ya sarafu ya kidijiti-Bitcoin.

Akizungumza na shirika la habari la Iran, amesema kuwa shughuli na Bitcoin zilizuiliwa na uamuzi wa baraza kuu la Fedha za kupambana na Blackchain. Nchini Iran, ni marufuku kuuza/kununua sarafu ya Bitcoin. Kupanda kwa thamani ya Bitcoin kumesababisha kupigwa marufuku kisheria ndio umeleta hilo. Niwashauri wananchi wasiingie katika mchezo huu~Bw. Nasir.

INAYOHUSIANA  Mwanzilishi mwenza wa Apple aamua kuikacha iPhone X

Naye, Bw. Ali Mueyyidi-rais wa Mamlaka ya Kupambana na Uhamiaji wa Bidhaa na Fedha za Kigeni, ameviambia vyombo vya habari kwamba shughuli zote zinazohusiana na Bitcoin zmeizuiliwa na wale ambao hawatokubaliana na marufuku hiyo watashughulikiwa.

Kwa mataifa mengi tuu na yenye uchumi mkubwa duniani lakini yamekuwa yakikumbana na vikwazo vya Marekani matumizi ya sarafu za kidijitali yameonekana kuwa kama mbadala wa nchi hizo kuweza kufanya biashara na hatimae kupata pesa kitendo ambacho kinakwenda kinyume na vizingiti vya kibiashara na uchumi kwa uumla vinavyowekwana nchi fulani.

Nchi kama Urusi, Iran, Venezuela na Uchina zimekuwa zikitumia sarafu za kidijitali kwa malengo ya kukwepa vikwazo ambavyo Marekani inaziwekea kutokana na sababu mbalimbali.

Iran

Sarafu ya Bitcoin

Kwa kiasi kikubwa marufuku hiyo inatokana na thamani ya Bitcoin kutokuwa ya kuitegemea kwa maana ya kwamba inaweza kupanda au kushuka kwa kasi hivyo kusababisha faida au hasara kwa wanaozimiliki.

Vyanzo: Coin Telegraph, CCN

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.