Katika vitu ambavyo siku hizi katika kufanya mawasiliano kwa njia ya maandishi kupitia simu, kompyuta, na kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi basi huwezi kuacha kuzungumzia emoji.
Apple ni moja kati ya makampuni ambayo yapo mstari wa mbele kutoa emoji mpya kila mwaka; yaani kama ni mwaka 2018 basi inakuja ‘Vikatuni’ hivyo vidogo tofauti na vile walivyotoa mwaka uliopita lakini swali rahisi ni je, kuna emoji zinazozungumzia watu wenye ulemavu?
Apple imepeleka mapendekezo kwa bodi inahusika kuidhisha emoji (Unicode Technical Committee) jumla ya emoji 13 yanayozungumzia ulemavu wa aina ambalimbali.
Emoji zilizopendekezwa na kupelekwa kwa jopo kwa ajili ya kupitiwa na kuidhinishwa baada ya kuonekana kukidhi kiwango ambacho kimewekwa na mamlaka husika kwa ujumla wake ni emoji 45. Emoji hizo zinaongelea mlemavu wa macho, mbwa anayemongoza mtu asiyeona, mlemavu wa kusikia mwenye kutumia kifaa maalum cha kumuwezesha kusikia, mlemavu wa kusikia kwa mbali, mlemavu wa viungo anayetumia baskeli ya kusukuma, n.k.
Ndani ya hizo emoji 45 zilizopendekezwa zipo pia emoji zinazozungumzia aina tofauti tofauti ya ulemavu wa ngozi.
Katika teknolojia ya emoji imekuwa haipo wazi sana kuwakilisha vyema kundi la watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali na iwapo mapendekezo ya emoji hizo yakipitishwa basi utegemee kuziona katikati ya mwaka 2019; emoji za mwaka 2018 zipo njiani kutoka.
Ulemavu upo wa aina nyingi lakini hakuna maneno yanayowaudhi walemavu hasa walioelimika unapomwita “Kilema”, “Kiwete”, “Kiziwi”, “Kipofu”, “Zeruzeru” na majina mengine yote ambayo si mazuri. Neno zuri na sahihi ni “Mlemavu wa ………..”.
Vyanzo: The Verge, Engadget
One Comment
Comments are closed.