fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao Teknolojia

Makampuni Ya Kiteknolojia Yenye Thamani Kubwa Zaidi Duniani! #2021

Makampuni Ya Kiteknolojia Yenye Thamani Kubwa Zaidi Duniani! #2021

Spread the love

Makampuni mengi ni matajari sana duniani, hapa hatuangalii utajiri bali tunaangalia thamani ya kampuni hiyo maana utajari unaangaliwa kwa njia nyingi sana, kama vile mapato, idadi ya wafanya kazi n.k

Katika orodha hii yameingia yale makampuni makubwa kabisa na yanajulikana kama nguli katika teknolojia.

 1. Apple Inc
 2. Microsoft
 3. Amazon Inc
 4. Alphabet Inc (Mmiliki wa Google)
 5. Facebook

Apple

apple ios

Apple

 • Mapato Ya Mwaka: $274 bln
 • Wafanyakazi : Watu 147,000

Apple inapewa thamani ya dola za kimarekani trilioni 2.169 na soko na mpaka leo ndio kampuni inayojihusisha na teknolojia ambayo ina thamani kubwa kuliko zingine.

Ukiachana na sekta ye teknolojia tuu kuna kipindi ilishika namba moja katika tasnia zote kama kampuni inayoongoza kuwa na thamani kubwa kuliko zingine.

Ni wazi kwamba Apple kwa mwaka wanaingiza faida ya mabilioni ya madola na hii inamaanisha kuwa ina wateja wengi na wana vifaa vizuri ambavyo wanauzia wateja hao.

SOMA PIA  Sailfish OS yawa Programu endeshaji rasmi ya simu nchini Urusi

Microsoft

udukuzi wa barua pepe

 • Mapato Ya Mwaka: $143 bln
 • Wafanyakazi : Watu 163,000

Soko linasema Microsoft thamani yake ni dola trilioni 1.611 za kimarekani, ambayo bado ni thamani kubwa sana.

Kampuni hii inamilikiwa na moja kati ya tajiri mkubwa sana duniani na huwenda akawa ndio tajiri maarufu maana amekaa katika orodha ya matajiri kwa muda mrefu (Bill Gates).

Kampuni ina bidhaa nyingi ikiwepo programu endeshi, kompyuta na vingine vingi ambavyo vinaifanya kuwa juu.

Amazon Inc

amazon

Logo Ya Kampuni La Amazon

 • Mapato Ya Mwaka: $280.5 bln
 • Wafanyakazi : Watu 798,000

Thamani yake kulingana na soko ni dola trilioni 1.569 za kimarekani, Hii ni moja katika ya kampuni kubwa sana na mmiliki wake kwa sasa (Jeff Bezoz) ndio tajiri namba moja duniani.

SOMA PIA  Faso Soap: Sabuni yenye kuzuia Malaria! #Sayansi

Kingine ukiangalia katika kampuni tano za kiteknolojia katika orodha hii utagundua kuwa Amazon ndio inayoongoza kuwa na rasilimali watu wengi kushinda kampuni zingine.

Kuna wengine wanaweza wakasema kuwa kampuni haijakaa kiteknolojia sana lakini usisahau kuwa kazi mama ya kampuni ni ile ya kununua na kuuza kupitia mtandao wake.

Alphabet Inc

Kampuni ya ALPHABET GOOGLE

Kampuni ya ALPHABET: Fahamu makampuni yaliyo chini yake

 • Mapato Ya Mwaka: $161 bln
 • Wafanyakazi : Watu 119,000

Soko linaipa Alphabet Inc thamani ya dola trilioni 1.171 za kimarekani, kumbuka kampuni hii ndio mmiliki wa kampuni ya Google Inc.

Mpaka sasa tovuti ya Google.com ndio tovuti maarufu na inayoongoza kutembelewa kuliko tovuti zote duniani.

Ukiachana na kampuni kuwa maarufu, bado inamiliki makampuni mengine mengi na pia ina miradi ya pembeni mingi ambayo inaifanya kampuni kubaki kuwa moja kati ya kampuni tajiri na yenye thamani kubwa.

SOMA PIA  TCRA: Tarehe ya kuzimwa simu feki haitasogezwa mbele

Facebook

 • Mapato Ya Mwaka: $71 bln
 • Wafanyakazi : Watu 45,000

Soko linaipa thamani  ya dola bilioni 670  za kimarekani. Facebook ndio mtandoa wa kijamii ambao ni maarufu kuliko mingine.

Ukiachana na umaarufu bado unabaki kuwa ndio mtandao wa kijamii mkubwa na mkongwe. Kampuni ina njia nyingi sana za kujipatie  fedha ikiwe ile ya kuuza matangazo katika mtandao wake.

Naaaaaam! hayo ndio makampuni ya kiteknolojia ambayo ni tajiri zaidi duniani, na mpangilio wako umeendana na thamani ambayo makampuni haya yamepewa na soko.

Kumbuka pia namba hizi (kiasi cha pesa wanazoingiza na thamani katika soko) vinaweza kushuka na kupanda muda wowote.

Niambie mpaka hapo unayaonaje makampuni haya? je nani atashuka na nani atapanda? ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania