fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Mtandao wa Kijamii

Makampuni Makubwa Ya Kiteknolojia Yatakiwa Kufungua Ofisi Nchini Urusi!

Makampuni Makubwa Ya Kiteknolojia Yatakiwa Kufungua Ofisi Nchini Urusi!

Spread the love

Urusi wamekuja juu wametoa agizo kwamba kwa makampuni makubwa (ya kiteknolojia) yote ambayo yanataka kuwa yanatangaza urusi kuwa na ofisi kule.

Hali hii inasemekana kuwa itasaidia kwa makampuni hayo kuepukana na kufungiwa baadhi ya matangazo yake na pia kusaidia kuepukana na penati ambazo zinaweza epukika.

Makampuni ambayo yanaguswa moja kwa moja ni yale makubwa kabisa na yanayojihusisha na mitandao ya kijamii. Mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, TikTok n.k hii inawahusu sana.

Baadhi Ya App Za Nchini Urusi

Baadhi Ya App Za Nchini Urusi

Sheria hii mpya imesainiwa kabisa na raisi wa urusi, Vladimir Putin. Sheria hii ni mahususi kwa makampuni ya kigeni ambayo yanajihusisha na internet kwa namna moja au nyingine.

Kingine ni kwamba kampuni hizo kubwa ni lazima ziwe zinatembelea na warusi zaidi ya laki tano kwa siku ndio sheria hii itaweza kuwagusa.

SOMA PIA  Intagram yaenda mbali, sasa inawatumiaji hai bilioni moja

Urusi ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa inasapoti sana App ambazo zinatengenezwa nchini humo humo, Mwaka 2019 ilitambulisha sheria ya kuamuru watengenezaji vifaa nchini humu kuzalisha vifaa vyao wakati tayari vikiwa vina App za urusi.

Baadhi Ya App Za Nchi Ya Urusi

Baadhi Ya App Za Nchi Ya Urusi

Urusi wanajitetea kwa kusema kuwa mitandao hii ikiwa na ofisi nchini mwao inakua ni rahisi kwa wao kuwa na rehani juu yao wakati lolote likitokea

SOMA PIA  Zlatan Ibrahimovic azindua game yake mpya ya Zlatan Legends

Kumbuka ofisi za Twitter nchini India zilizungukwa na maaskari baada ya kutokea moja ya tweet ya mwanasiasa kudaiwa kuwa picha ambata ilipikwa.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii unaichukuliaje? je ni jambo zuri au unaona halina maana yoyote?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania