fbpx

Sony, Teknolojia

Magemu ya kucheza kwenye PS5 kugharimu zaidi ya Tsh. 158,000

magemu-ya-kucheza-kwenye-ps5-kugharimu-zaidi-ya-tsh-158-elfu

Sambaza

Kwenye ulimwengu wa magemu hivi sasa dunia inaimba kuhusu PlayStation 5 ambayo mengi tuu ulimwengu umeshafahamu na kifaa hicho kinakuwa na mantiki ndogo sana pasipo na uwepo wa magemu.

Kwa haraka haraka PlayStation 5 (PS5) ni kifaa ambacho kinatengenezwa na Sony Corporation kinatumika kama kiburudisho kwa kucheza michezo iliyo katika mfumo wa picha za mnato. Uwezo wa kifaa hiki kwa maana ya diski uhifadhi ni GB 585, GB 16 za RAM.

Sasa ingawa watu wengi wanasubiri uzinduzi wa PlayStation 5 ambao utafanyika Novemba 19 2020 tufahamu ya kuwa bei yake tu itaanzia $399|zaidi ya Tsh. 917,000 ikiwa haina gemu, $499|zaidi ya Tsh. 1,147,700 (ikiwa na gemu moja).

PS5
Hiyo ndio PlayStation 5 (PS5) inayoonekana kuongelewa na wengi duniani.

PalyStion 5 ama hizo zilizopita hazivutii kama hazina magemu na kwa habari zilizopo ni kwamba gharama yake itafikia zaidi ya 158,000 pesa ya Tanzania (zaidi ya $69). Magemu yanayozungumzwa sana ni Spider-Man: Miles Morales kwa $49.99 na toleo jingine litapatikana kwa $69.99 bei ya ughaibuni.

INAYOHUSIANA  Guccifer: Mdukuzi aliyewahi kumdukua Bush ahukumiwa jela
PS5
baadhi ya magemu ambayo mtu anaweza kucheza kwenye PlayStation 5.

Haya sasa wale wapenzi wa PlayStation tumejipangaje? Sasa umeshapata habari basi ni vyema ukaongeza nguvu ya mfuko wako kama ulikuwa umetenga kiasi kidogo ili kuweza kuinunua.

Vyanzo: The Verge, PlayStation Blog

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Farm Ville: Mwisho wa gemu hili umefika! - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    September 29, 2020 at 6:07 pm

    […] kabisa wewe ukawa ni mmoja kati ya watu wengi duniani ambaao wanacheza gemu/magemu kama sehemu ya kujiburudisha, kuingiza kipato, n.k kupitia simu janja, kompyuta au kifaa […]

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*