fbpx

Maboresho kwenye teknolojia ya kuhakiki mizigo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

vodacom swahili

Sambaza

Usalama ni kitu muhimu sana na imekuwa ni jambo la kawaida kuona uwekezaji/kuboreshwa kwa teknolojia mbalimbali kama njia ya kujihakikishia mzigo fulani hauna kitu kibaya.

Uwanja wa ndege wa JFK uliopo jiji la New York umeamua kubadilisha teknolojia ya uhakiki wa mizigo wa abiria wanaoiniga na kutoka kiwanjani hapo; awali teknolojia ya X-ray ndio ilikuwa ikitumia kukagua mizigo lakini mashine ya CT scan imeonekana ikifungwa kiwanjani hapo na kuanza kutumika.

Kwanini iwe CT Scanner badala ya X-ray?

Katika teknolojia ya kuangalia kilichopo ndani ya mzigo wa abiria CT scanner imeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kuona kilichopo ndani bila ya kuchambua vitu mathalani viminika, vifaa vikubwa vya kielektriniki, n.k bila ya kuvitoa.

MAshine hizo za CT scan tayari zinafanyiwa majaribio katika miji ya Phoenix na Bosoton. Kwa mwaka 2018 kiwanja cha ndege JFK kitafungwa mashine 15 za CT scan.

Vilevile, mashine ya CT scanner imeonekana kuweza kuona mzigo kwa ndani vizuri zaidi kulinganisha na X-ray ambapo imeelezwa kuwa CT scanner ina uwezo wa kuuzungusha mzigo katika nyuzi 360 na kuweza kutambua vifaa hatari kama vilipuzi kwa upana zaidi jambo ambalo ni muhimu sana katika kupambana na uhalifu/ugaidi.

teknolojia ya kuhakiki mizigo

Mashine ya CT scan ikitumika katika kazi tofauti na ile iliyozoeleka.

Katika miaka mitano ijayo inaaminika kuwa abiria hatohitaji kutoa baadhi ya vitu kwenye begi lake ili ukaguzi uweze kufanyika vyema. Nchi zetu za Afrika zinazoendelea inatakiwa twende huko kama njia mojawapo ya ukaguzi wa mizigo.

Chanzo: Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Karma: Falme za Kiarabu ilidukua simu za iPhones nyingi za wapinzani wake! #Skendo
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.