Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

apps, Google, Picha, Teknolojia

Maboresho: Huduma ya Google Photos yazidi boreshwa

maboresho-huduma-ya-google-photos-yazidi-boreshwa

Sambaza

Google Photos imefanyiwa maboresho ambayo yalitangazwa katika mkutano wa I/O siku chache zilizopita, maboresho hayo ni pamoja na kuja uwezo wa kuwa-tag watu katika picha na pia uwezo wa kuzihifadhi picha ili zisionekane katika ukurasa wa kawaida.

google photos

Google Photos ni app ya Google ambayo inajikita zaidi katika kuhifadhi picha zako unazopiga katika simu, app hii inarahisisha pia kupata picha ulizopiga zamani ambazo zimehifadhiwa.

Google Photos kwa sasa imepewa uwezo wa kuzificha (ama archive) picha, kipengere hichi kinaweza tumiwa pale ambapo tunataka picha fulani zisionekane pindi tukiwa tunatumia app hii mfano unapicha za mtoto mdogo ambazo bado hautaki watu wazione basi ukizificha hazitatokea katika ukurasa wa kawaida wa app (kumbuka picha ukiziarchive bado zinapatikana katika kurasa ya albamu).

SOMA PIA  Andorid Pie yaenea zaidi kuliko Oreo

google photos
Muonekano mpya wa menyu ya Google Photos iliyoboreshwa.

Google pia wameleta uwezo wa kutag watu katika picha zako (kama tunavyo fanya katika Facebook), marafiki zako sasa wataweza kukutag katika picha ambazo wanasambaza na wewe utazipata picha hizo kirahisi zaidi.

Pamoja na mengine Google Photos pia wameboresha teknolojia ya kutambua sura katika picha hivyo kwa sasa ni rahisi kuzipata picha zako kwa kutafuta jina lako tu na sio lazima kuanza kutafuta kwa kufungua picha zako zote.

SOMA PIA  Download Mp3 na Video kutoka YouTube kwenye simu za Android

Je umekwisha wahi tumia hii app? kama unaitumia tuambie maoni yako juu ya maboresho haya na kama hauitumii tunakushauri ujaribu kuitumia kwani pamoja na yote ni moja kati ya app ambazo zinakusaidia usipoteze picha ama meme zako ulizonazo katika simu hata kama simu itapotea.

SOMA PIA  Mambo/Maboresho ambayo Apple wanayafanyia kazi

Endelea kufuatilia mtandao wako wa Teknokona kwa habari motomoto za Teknolojia, pia tufuate katika mitandao ya jamiii kama Facebook Twitter na Instagram.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Sambaza

Nickson

    1 Comments

    1. Apps na Programu za Google Drive na Google Photos zatenganishwa
      June 15, 2019 at 12:43 am

      […] Drive na Google Photos zatenganishwa na Google. Google wamefanya uamuzi huo wakisema unatokana na maoni ya utumiaji ambao […]