fbpx
Magari, Teknolojia, Uganda, Usafiri

Uganda: Mabasi ya umeme Jua kuanza kutengenzwa kwa wingi

mabasi-ya-umeme-jua-kuanza-kutengenzwa-kwa-wingi
Sambaza

Ukitaka kukabiliana na suala zima la uchafuzi wa mazingira basi ni lazima ufikirie kutumia nishati mbadala. Uganda wanaaziwa kuanza kutumia magari yanayotumia umeme wa Jua kabla ya mwisho wa maka huu (2019).

Serikali itaanza kufanyia majaribio mabasi hayo mwaka huu na kwamba serikali iko tayari kutoka shilingi za Uganda bilioni 143 kusaidia utengenezaji wa magari nchini humo.

Mwaka 2014 mamlaka ya uwekezaji ya Uganda ilitoa kandarasi kwa kampuni mbili – Kiira Motor inayomilikiwa na Chuo Kikuu cha Makerere na China Engineering kuanza uzalishaji wa magari mwaka 2018.

Umeme Jua
Basi hilo linalotumia umeme wa Jua lilizinduliwa mwaka 2016 likipewa jina la ‘Kayoola Solar Bus’.

Kayoola lina na viti 35 vya abiria pamoja na kuwa na betri mbili; moja inachajiwa kwa umeme Jua na nyingine kwa umeme wa kawaida. Betri inayotumia umeme Jua ikichajiwa itakuwa na uwezo wa kutembea kilomita 80 kabla ya kuchajiwa tena. Aidha, betri nyingine ya umeme wa kawaida itakuwa ni kwa ajili ya matumizi ya safari za usiku.

INAYOHUSIANA  Samsung Galaxy S9/S9+ yapokea Android Pie
Umeme Jua
Matarajio ya kiwanda hicho cha utengenezaji wa mabasi hayo ni kwamba ifikapo mwaka 2039 itakuwa na uwezo wa kuzalisha vifaa vyote ndani ya Uganda badala ya kutegemea kununua baadhi ya vipuri kutoka nje ya nchi.

Basi moja linatarajiwa kuuzwa kwa dola za kimarekani 40,000. Mradi huu wa mabasi ya umeme Jua unasimamiwa na kampuni ya Kiira Motors inayomilikiwa na serikali ya Uganda.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.