fbpx

Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Samsung ni kampuni ambayo ina watumiaji wengi wa simu janja, licha ya hivyo ni kampuni ambayo inajitahidi kuja na teknolojia ya juu katika vifaa vyakokwa sasa iko na Galaxy S10.

Toleo lake la Galaxy S10 limetoka tayari na hivi sasa ni muda mzuri kwao katika kulitangaza toleo hilo. Kwa upande wao wamekuja na njia tofauti za kutangaza vifaa vyao ukilinganisha na makampuni mengine.

Bango Ambalo Ukisogeza Karibu Galaxy S10 Basi Itaweza Kuingiza Chaja Ambalo Lipo Katika Kituo Cha Basi Singapore

Huko nchini Singapore katika vituo vya mabasi ambavyo havikaukiwi na watu kwa kiasi kikubwa wameweza kuweka mabango spesheli kwa kushirikiana na kampuni ya matangazo ya JCDecaux. Mabango haya watumiaji wa Galaxy S10 wanaweza kuyatumia ili kuchaji vifaa vyao bila chaji.

INAYOHUSIANA  BlackBerry Messenger (BBM) kufungwa Mei 31

Kumbuka Galaxy S10 inakuja na uwezo wa kuweza kuchaji simu hiyo bila ya kutumia kimemeshi. Vituo hivyo vinajulikana kama “Power sharing stations.

Lakini jambo kama hili sio la kushangaza sana kutoka kwao Samsung kwani wameshawahi hata kuleta teknolojia kama hii; wiki kadhaa tuu zilizopita waliweza kutumia teknolojia hii katika mabango hayo huku wakiwa wanatangaza ni jinsi gani teknolojia ya kuchaji bila chaja kunafanya kazi.

Bango Ambalo Ukigusogeza Karibu Galaxy S10 Basi Itaweza Kuingiza Chaja

Bango Ambalo Ukisogeza Karibu Galaxy S10 Basi Itaweza Kuingiza Chaja

Kwa jambo hili kampuni tunaipongeza sana maana inajitangazia biashara ya simu husika wakati na watumiaji wa simu hizo wanafaidika vilivyo na teknolojia hiyo endapo simu zao zitakua zimeishiwa na umeme lakini pia kama watakua meneo ya karibu na vituo hvyo.

INAYOHUSIANA  Huawei Mate 20X ya 5G yaingia sokoni

Teknolojia hii inaonekana kama ina tija na watu ambao washaanza kuitumia wametokea kuipenda, kuna hati hati kubwa teknlolojia hii ikaendelea kutumia hata katika maeneo mengine duniani.

Tembelea Teknokona Kila Siku Ili Kuendelea Kupata Habari Kedekede Zinazohusika na Teknolojia Kwa Ujumla, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.