Je ushawahi kujiuliza maana ya i katika iPhone na iOS? Kwa nini Apple wanatumia herufi i katika kutambulisha bidhaa zake kama iPhone, iPad, iPod na programu endeshaji ya iOS? Leo fahamu.
Lakini kuelewa maana ya herufi hiyo kwa kuzingatia iPhone, inabidi turudi nyuma hadi wakati wa kwanza Apple ilipotumia “i” katika majina ya bidhaa zake. Kifaa kingine cha Apple kilicholeta mapinduzi makubwa ndicho kilichokuwa cha kwanza kutumia “i” — kompyuta binafsi ya iMac.
iMac ya kizazi cha kwanza yenye rangi za kuvutia iliingia sokoni mwaka 1998, mwaka mmoja tu baada ya Steve Jobs, mwanzilishi wa Apple, kurudi kama Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo. Katika uzinduzi wa bidhaa hiyo mwaka huo, Jobs alithibitisha kuwa herufi ndogo “i” katika iMac haikuwa na maana moja tu, bali tano.
Maana ya kwanza ni intaneti, ambapo Jobs alieleza kwamba sababu kuu ya watu kutaka kompyuta nyumbani ilikuwa kuunganishwa na ulimwengu mpya wa mtandao wakati huo. Baada ya hapo, Jobs alitaja maana nyingine nne za “i” kuwa ni individual (mmoja mmoja), instruct (kufundisha), inform (kutoa taarifa), na inspire (kuhamasisha).
Kwa kiasi kikubwa hii ilimaanisha kupitia kifaa cha Apple, mtu mmoja mmoja atakuwa na uwezo wa kufundisha, kutoa taarifa na kuhamasisha – yote yakiwezekana pia kupitia teknolojia ya intaneti. Mtumiaji yoyote katika utumiaji wake wa kifaa cha Apple kuna namna moja au zaidi ya i moja zinamgusa.
No Comment! Be the first one.