Katika maisha baada ya kuheshimu Mungu wetu, wazazi kitu kinachofuata ni muda kwani bila ya hivyo vitu vinakuwa haviendi kwa mpangilio. Kuwa katika ulimwengu wa kiteknolojia kumerahisisha mengi lakini bado saa hazijasahaulika ila zinazidi kuboreshwa.
Sasa katika ulimwengu wa kidijiti tumeshasikia na pengine kuziona saa nyingi sokoni lakini ni ukweli usiopingika kuwa saa za Apple ni marufu sana kutokana na ubora na ulimwengu wa teknolojia unataka nini kwa wakati huo.
Msingi wa kulifanya betri za kidijiti zidumu zinategemea sana na mfumo endeshi ambao umewekwa huko kwa wakati huo. Makala hii inazilenga saa za Apple ambapo mbali na hivi juzi tuu kutoa iOS 14 pia kwenye upande wa saa kuna watchOS 7.
Kama una saa ya Apple na umeshaboresha na kuweka watchOS 7 kuna namna ya kufanya betri la kwenye kifaa husika kiwe na maisha mrefu; kwenye toleo hilo la programu tumishi kuna kipengele kinaitwa “Optimized Battery Charging“.
Mbinu ya kutumia kufanya betri ya Apple Watch idumu
Inaweza kuwa ni tabia ya wengi kuweka vifaa vyetu kwenye chaji nyakati za usiku tukiwa tumepumzika. Iwapo kipengele cha “Optimized Battery Charging” kimeruhusiwa (kama Apple Watch inatumia watchOS 7) basi itajaza umeme mpaka kiwango fulani na kuacha kiasi kidogo ambacho kitafikia mwisho (kujaa kwa asilimia 100) kabla hujaamka.
Mfano umeweka saa yako ya Apple kwenye umeme na umechagua iwake saa moja asubuhi basi fahamu ya kuwa itajaza chaji mpaka asilimia 80 na kuacha kwa muda wa saa 1-2 ili kuweka zile 20% ambazo zimebakia; kwa lugha rahisi ni kwamba mpaka saa itaacha kuchaji muda wowote ambao itakuwa imefikia 80% na kuja kuendelea kati ya saa 11 alfajiri au saa 12 asubuhi ili mtu atakapoamka saa 1 asubuhi anakuta imejaa kwa 100%.
Mbinu ya kutumia kuifanya betri la kwenye Apple Watch imudu.
Kwanini inashauriwa na jinsi ya kuipanga
Uzuri wa kuwasha kipengele cha “Optimized Battery Charging” inasaidia kufanya afya ya betri nzuri kwa sababu inapunguza muda wa saa kujaa chaji mpaka asilimia 100 kutokana na kuwa kwenye umeme kwa muda fulani kisha kusimama halafu kuendelea tena baada ya muda fulani.
Kama simu tayari inatumia watchOS 7 basikipengele hicho kinakuwa kimeweshwa tayari na kama hupendezwi nacho; unapenda muda wowote utakaoamka (kabla ya muda uliojiwekea) ukute imeshajaa tayari itakubidi kufuata hatua zifuatazo kuwasha/kuzima kipengele husika:-
>Bofya kitairi cha upande wa kulia kwenye saa ya Apple ili kuleta menyu,
Hatua ya kwanza kuweza kuwasha/kuzima kipengele cha kufanya betri ya Apple watch idumu.
>Kisha nenda Settings>>Battery>>Battery health>>Optimized Battery Charging>>Turn Off au Turn Off Until Tomorrow.
Hatua ya pili kuweza kuwasha/kuzima kipengele cha kufanya betri ya Apple watch idumu.
Kitu chochote ili kidumu kinahitaji matunzo mazuri hivyo basi tuzitunze saa zetu za kidijti ili muda wote uweze kuona thamani ya pesa uliyotumia kununua kifaa/bidhaa husika.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
One Comment