fbpx

Huawei Wapewa Dili La Teknolojia Ya 5G Licha Ya Kashfa Kutoka CIA!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

TeknoKona iliandika kuhusu Huawei Kushutumiwa vikali na chombo cha CIA kwamba wanapokea misaada ya kifedha kutoka katika mashirika mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine yanajihusisha na ulinzi na usalama kwa kushirikiana na serikali ya China.

Ingia  hapa kusoma andiko la mwanzo

huawei wazuiwa marekani

Logo Ya Huawei Kwa Mbali

Licha ya kashfa zote hizo na vikao vingi vilivyokaliwa ili kulijadili hili waziri mkuu wa uingereza, Theresa May ametoa ruhusa kwa mtandao huo kuendelea na mkataba. Mkataba huo unahusisha Huawei kutengeneza vifaa kama vile antena na vifaa vingine ambavyo vitaruhusu na kutumia teknolojia ya 5G.

INAYOHUSIANA  Unajua undani wa Honor V20?

Mawazo hao yamefikiwa licha ya kwamba Huawei bado inadhaniwa inaweza ikaleta matitizo makubwa katika swala zima la ulinzi na usalama …kulingana na maelezo ya CIA na vyombo vingine ambavyo viliongelea swala hili.

Imani yetu ni kwamba mpaka taafa kubwa limefikia maamuzi kama haya ya kuiacha kampuni hiyo kuendelea na mkataba wake wa kuhakikisha teknolojia hiyo inafanya kazi kwa ufasaha, ni kwamba uchunguzi wa kina sana umefanyika juu ya jambo hili.

INAYOHUSIANA  Huawei yajigamba na Kirin 980

Kumbuka kwa chini wanaongoza kusamba na kutengeneza vifaa vya kieletroniki — ukiachana na simu — ni kampuni mbili ambazo ni Huawei na ZTE. Vilivile Huawei bado wanapigana mahakamani na serikali ya marekani kwani kuna baadhi ya vifaa vyake vimekatazwa kutumika katika maofisi. Pingamizi hilo linakuja kama sehemu ya Huawei kutaka watu wajue kwamba hawana nia mbaya kabisa.

Comment zilikua nyingi sana lakini moja iliyonivutia ni kwamba inawezekana kuwa Huawei kweli anaweza akawa ana nia mbaya ya kuharibu ulinzi na usalama au kwa upande mwingine asiwe na nia hiyo. Lakini ukifikiria kwa undani ni kwamba Kampuni yeyote inayotengeneza vifaa vya kielektroniki na kiviuza katika masoko makubwa bado inaweza ikawa na nia mbaya na taifa lolote.

INAYOHUSIANA  Simu za Huawei kuja na apps 70 maarufu kuepuka vikwazo vya Marekani

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini. Kumbuka kutembelea TeknoKona kila siku ili ujipatie habari kem kem zinazohusiana na teknolojia na sayansi kwa ujumla. TeknoKona tupo nawe!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.