Je unafahamu kwa nini Facebook inatumia rangi ya bluu kwenye ubunifu wa app na tovuti yake?
Vingi vina rangi lakini katika maswala ya tovuti ni muhimu sana kuchagua rangi ambayo kwa namna moja au nyingine itaendana na mtandao husika. Kingine ni kwamba hata kama baadhi yetu hatujui ni kwamba kila rangi ina maana yake mbele ya macho ya watu.
Facebook wamelizingatia hilo kwa kuweka rangi ya bluu katika mtandao hio lakini cha kujiuliza ni kwamba ni kwanini mtandao huo una rangi ya bluu? kwa nini isingekuwa rangi nyingine?
Ni wazi ili kufanya mtandao/tovuti kuvutia sana watu, na iwe ya kirafiki zaidi ni lazima rangi izingatiwe sana. Wakati Facebook inatengenezwa muanzilishi wake rangi ambayo alikuwa nayo katika akili yake ilikua ni rangi ya bluu,
Ukiachana na hilo kwani hata wewe hujawahi kujiuliza kwanini mtandao huo una rangi hiyo tuu? kwanza, kwa taarifa yako ni kwamba rangi hiyo ya bluu ina maana ya Amani hili lina maana kubwa sana kwani kumbuka kazi kubwa ya mtandao huo wa kijamii ni kuunganisha dunia nzima katika mawasiliano.
Ukaichana na amani bado rangi ya bluu inaonyesha hadhi ya utulivu na ni moja kati ya rangi bora kabisa dunaini. Sifa za rangi hii ndizo pekee ambazo zimemfanya muanzilishi wa Facebook kuichagua rangi hii.
Tangia Facebook ianzishwe 2004 mpaka leo ni vipengele vingi sana vimebadilika lakini katika swala la rangi hawajagusa kabisa, hivyo basi hakuna mabadiliko yoyote juu ya hilo.
Kingine ni kwamba muanzilishi wa facebook ameshawahi kunukuliwa akisema “BLUE IS THE RICHEST COLOR FOR ME – I CAN SEE ALL OF BLUE.” — kwa tafsiri ya haraka haraka ikiwa inamaanisha kuwa bluu ndio rangi ambayo anaielewa sana kwani anaweza akaiona vizuri zaidi