fbpx
apps, Google, Google Map, Maujanja

Fahamu jinsi ya kukimbia foleni kwa kutumia Google Maps

kutumia-google-maps-app-foleni
Sambaza

Je, umeshagundua kuna njia rahisi ya kukimbia foleni kwa kutumia Google Maps? Iwe kwenye app ya simu au kompyuta unaweza kutumia huduma ya Google Maps kufahamu muda utakaokuchukua kufika unapotaka kwenda.

Kupitia Google Maps unaweza kupata:-

  • makadirio ya muda utakaokuchukua kufika sehemu iwe kwa njia ya miguu, gari, n.k,
  • ushauri wa njia za kupita, utapewa njia mbadala pamoja na wastani wa muda utakaokuchukua kufika,
  • kama njia zina foleni basi utaweza kutambua foleni hizo zipo maeneo gani na wastani wa muda itakuchukua kwenye vipande husika vya foleni.

Kitu kizuri kwenye huduma ya programu tumishi ya Google Maps ni kwamba itaweza kutambua na kukumbuka tabia za safari zako na hivyo kukupatia makadirio hayo kwa usahihi zaidi kila unavyoitumia.

INAYOHUSIANA  Facebook Wampa Mtoto wa Miaka 12 Dola $10,000 kwa ku'hack Instagram

Je, ni jinsi gani ya kunufaika au kutumia Google Maps kwa ajili ya usafiri?

Kutumia Google Maps
Kutumia Google Maps: Mfano wa ushauri wa njia kutoka Oysterbay kwenda Tegeta

> Kwa safari za mara moja

Fungua app ya Google Maps app Google Maps kutumia Google Maps

  • Tafuta eneo unalotaka kwenda kupitia kutafuta (search) au kwa kuchagua kwa kugusa eneo kwenye ramani
  • Katika eneo la chini bofya ‘Directions‘ – yaani kupewa maelekezo ya sehmu unayokwenda
  • Katika eneo la juu kidogo bofya ‘Drivingkutumia Google Maps– hapa ni kusaidia Google kujua aina ya usafiri utakaotumia. Ukibofya eneo la chini jeupe utapata taarifa nyingi zaidi za safari yako kama vile muda utakaochukua kwenye foleni za mbele pamoja na mengineyo.

> Kwa safari za mara kwa mara

Kama tayari umeshawahi kuweka chaguo la eneo la makazi/nyumbani pamoja na eneo unalokwenda mara kwa mara kama vile kazini unaweza kubofya eneo la “Commute” na moja kwa moja Google watakupatia makadirio ya safari unazofanya mara kwa mara.

INAYOHUSIANA  Snapchat Waanzisha Ma'Group' Na Vipengele Vingine, Sasa Chat Mpaka Na Watu 16!

Kama bado haujaweka taarifa za makazi na eneo unalokwenda mara kwa mara kama vile kazini au chuo basi unaweza fanya hivyo na uzuri ukifanya hivyo Google wataweza kukutumia taarifa mara kwa mara baada ya kugundua muda ambao huwa unatoka eneo moja kwenda jingine.

Kwenye Google Maps.

  1. Bofya Commute kutumia Google Maps.
  2. Bofya More(juu kulia kwenye nukta 3) More Settings and then Commute settings and then How you commute and then Weka/Fanya masahihisho ya taarifa za safari
INAYOHUSIANA  Uwezo wa kuchati kwenye Youtube kuondolewa kabisa!

Kuweka kumbukumbu za eneo ambalo ni nyumbani au kazini

  1. Fungua app ya Google Maps kutumia Google Maps.
  2. Bofya/Nenda Menu Menu and then Your places.

Kufanya mabadiliko ya taarifa za sehemu: Bofya More More and then Edit [Sehemu].

Katika kufanikisha huduma hii Google inatumia data za watumiaji wengine wa huduma za Google kwenye simu zao ambao wanakuwa kwenye njia husika kwa wakati huo. Huduma ya Google Maps kwenye usafiri inanufaika sana na data za GPS zinaochukuliwa kutoka maelfu ya watumiaji wa huduma za Google.

Je, kuna maujanja gani unataka kufahamu kuhusu huduma zinazopatikana kwenye programu tumishi unazotumia zaidi? Tuambie kwenye sehemu ya kutoa maoni.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |