Kutokana na ukuaji wa teknolojia wataalam mbalimbali wameendelea kutafuta njia zaidi ya moja ambayo itamuwezesha mtu kufanya kitu kilekile ambacho anaweza kukifanya kwa kutumia simu.
Tukiwa tukaribia kumaliza mwaka 2018 Google waneleta maboresho kidogo katika kuwarahisishia watumiaji wa rununu za Android kuweka kutuma/kujibu ujumbe mfupi wa maandishi kupitia tovuti ambapo itakubidi utumie kivinjari kuweza kuifikia.
Kama ambayo tunafahamu kuwa kuna WhatsWeb basi kitu kama hicho kimeletwa upande wa vifaa vya Android ili kuweza kujibu jumbe zilizotumwa kwenye simu yako kupitia TOVUTI MAALUM lakini itakubidi kuunganisha kati ya simu ya Android na kifaa kingine mathalani kompyuta ili kuweza kuleta mawasiliano kati ya vifaa hivyo viwili.

Kwa wale ambao tunapenda kutumia kompyuta hasa kwa huduma za WhatsWeb, hii ya kujibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia tovuti ni kitu kingine cha kuvutia.
Vyanzo: GSMArena, Economic Times