fbpx

Kutopatikana kwa Google Allo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Google wanafahamika kwa vitu vingi ambavyo watu wenye simu za Android wanatumia kwenye vifaa vyao lakini polepole tunaanza kuona programu mbalimbali zikiondolewa kwa maana ya kwamba kutopatikana kwenye soko la programu tumishi/kutoweza kutumika tena na mojawapo ya programu hizo ni Google Allo.

Sisi kama wafuatiliaji wa habari zinazohusu teknolojia tulishawahi kuleta mbele ya macho ya wasomaji wetu kuhusu Allo-programu tumishi iliyomuwezesha mtumiaji kuweza kuwasilianakwa njia ya maandishi/picha jongefu na kupata umaarufu wake lakini sasa Google wameamua kuiondoa kwenye matumizi ambayo haijapokea masasisho tangu mwezi Januari 2018.

INAYOHUSIANA  Mawasiliano ya Skype yanayohusisha watu wengi zaidi

Kwanini Google Allo imetolewa?

Wakati inazinduliwa mwaka 2016 lengo la kuleta programu tumishi husika ilikuwa ni kuleta ushindani kwa programu kama vile WhatsApp, Telegram, LINE, Viber lakini mambo yamekwenda ndio sivyo na mwezi Desemba mwaka jana wakaweka wazi Machi 2019.

Tangu mwezi Desemba mwaka 2018 Google walitoa uwanja watu kuweza kutunza mazungumzo yao kwenye programu tumishi ya Allo ambayo haipatikani tena tangu Machi 12 2019.

Google Allo

Allo iliamualiwa kusitishwa kutokana na kushindwa kuleta matarajio kama ambavyo Google walitarajia.

Huoni muendelezo wa Google kuachana na programu tumishi ambazo zimepoteza ushindani; mwezi Aprili Google Hangouts nayo itaondolewa hivyo basi tunakushauri kutunza kumbukumbu ya mazungumzo ambayo usingependa yapotee kabla haijafungwa.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.