BlackBerry kama kampuni wamejiweka pembeni kuhusu biashara ya simu janja tangu mapema mwaka 2020 lakini inaweza kuwa ngumu kwa jina hilo kupote sokoni kwani kuna makampuni wana nia ya kuirudisha kwenye ushindani.
Katika kufanya tuje kuona simu janja za BlackBerry hasa zinazotumia 5G Onward Mobility imeamua kubeba mikoba ya waliamua kuiacha tangu mwezi Agosti 2020 na kujipanga kutoa rununu ambazo zina teknolojia hiyo ya kisasa ya mawasiliano kwa sasa.
Onward Mobility wameamua kuja na mtindo mpya kabla ya kutoa aimu hizo janja za BlackBerry ambapo wameanzisha programu maalum inayoshirikisha orodha ya wabia, wadau wa BlackBerry ambao wanapata kupewa bidhaa, kutoa mapendekezo na hata dondoo ya hicho ambacho kinatengenezwa kabla ya kultwa kwa kadamnasi.

Je, hii inatoa taswira gani?
Kwa lugha rahisi hapa maana yake ni kwamba simu janja mpya za BlackBerry zipo tayari kutoka na kampuni hiyo kuweka wazi kuja na ambazo zinatumia teknolojia ya 5G.

TCL nao walitoa simu janja kwa ushirikiano na nguli hao wa programu wezeshi kwenye masuala ya ulinzi na usalama lakini safari hii Onward Mobility wapo wenyewe na wameahidi kuja na simu janja mwaka huu baada ya 2021 kuwa na changamoto nyingi zilizosababisha mambo kutokwenda sawia. Je, itakuaje? Salia nasi na tutakuhabarisha.
Vyanzo: GSMArena, Notebook Check
No Comment! Be the first one.