Katika dunia ya leo ambayo ipo kidijitali zaidi kuna njia mbalimbali za mtu kuweza kufika mahali mpaka ulipo na hii inatokana na kipengele muhimu sana kwenye Google ambacho kinasaidia kitu fulani kionekane kwenye ramani.
Si haba unaweza ukawa unamiliki biashara ambayo inafahamika na wengi kutokana na kwamba umeitangaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho sio kibaya kabisa lakini itakuaje kwa yule ambae hafahamu biashara yako ilipo? Hapo ndipo linapokuja suala zima la kuifanya mahali ilipo ofisi ifikike kirahisi hata kwa yule anayetumia mwongozo wa Dira.
Unaweza kuwa umeona kwenye tovuti mbalimbali zikionyesha mahali ambapo ofisi husika ilipo basi tambua ya kuwa kuna hatua zilifuatwa mpaka eneo husika likaweza kuonekana kwenye ramani:
Hatua ya kwaza: tembelea maps.google.com kisha wengiza anwani ya eneo/mtaa ambapo ofisi yako ipo kisha bofya “Enter“.
Htua ya awali ni kutafuta mtaa ambao ofisi husika ipo.
Hatua ya pili ni kurekebisha/kujaza (bofya palipoandikwa suggest edits>>change name or other details) taarifa kamili za ofisi/biashara husika. Hapa ndipo utakapotakiwa kujaza jina la kampuni /biashara, anwani ya mtaa, saa za kazi, namba ya simu, tovuti (ambayo ipo hewani tayari), n.k.
Baadhi ya taarifa ambazo utatakiwa kujaza pale unapotengeneza ramani ilipo biashara/ofisi yako.
Hatua ya tatu ni kusambaza kwa watu. Hii itasaidia kuwafahamisha wateja ni wapi ilipo biashara yako na kuweza kufika bila shida yoyote/kusumbuka ukitafuta ofisi ilipo.
Ukitaka kufikia watu wengi huna budi kuwafahamisha na wengine.
Kwa kuhitimisha kabisha unaweza ukanakili anwani kutoka kwenye ramani ya Google kisha ukaiweka kwenye tovuti na mtu akawa na uwezo wa kufika mahali ambapo biashara ipo.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|