fbpx
Google

Kuna nia ya kuitenganisha Google na biashara yake ya matangazo. #Marekani

kuna-nia-ya-kuitenganisha-google-na-biashara-yake-ya-matangazo-marekani

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Wanasheria wakuu wa baadhi ya majimbo nchini Marekani waangalia kama kuna ulazima wa kuilazimisha na kuitenganisha kampuni ya Google na biashara yake ya matangazo ya mtandaoni.

Suala hili linatokana na uchunguzi juu ya shutuma za kujipendelea dhidi ya Google zinazotolewa na makampuni mengine.

Inasemakana kutokana na Google kumilika biashara na mfumo mkubwa wa matangazo ya mtandaoni basi wamekuwa wakizipendelea baadhi ya bidhaa zake hasa hasa katika kutokea zaidi katika huduma ya utafutaji ya Google Search.

INAYOHUSIANA  Vitu Vilivyotafutwa Zaidi - Google Mwaka 2014
kuitenganisha Google na biashara yake ya matangazo
Kuitenganisha Google na biashara yake ya matangazo: Huduma ya matangazo ya Google inahusisha matangazo katika huduma ya utafutaji, kwenye tovuti mbalimbali na YouTube.

 

Mpango huu umeripotiwa na vyanzo kadhaa na kuthibitishwa na chombo cha habari cha Marekani cha CNBC. Ofisi za Wanasheria wakuu katika majimbo mbalimbali zimeshafungua uchunguzi dhidi ya Google kujipendelea katika huduma ya utafutaji ya Google Search, mfumo wake wa matangazo na kwenye programu endeshaji ya Android.

Msemaji wa Google amesema wanatoa ushirikiano wote unaohitajika na bado wanaendelea na msimamo ya kwamba hakuna upendeleo wowote unaoendelea.

INAYOHUSIANA  Rasmi: Android O, sasa ni Android 8.0 Oreo :-)

Ni kawaida kwa makampuni yenye biashara nyingi na kujikuta yanaongoza katika kila maeneo yanayojishighulisha kujikuta katika uchunguzi na kesi za kutoruhusu wengine kunufaika na huduma zao. Ata makampuni mengine kama Amazon, Apple, na Facebook wanachunguzwa katika maeneo mbalimbali chini ya sawa la haki za kibiashara za ushindani.

Tutaendelea kufuatilia maendeleo ya uchunguzi na matokeo yake, endelea kutembelea TeknoKona na kumbuka unaweza ungana nasi Telegram kwa mazungumzo mbalimbali ya Teknolojia kwa kubofya hapa Telegram -> @teknokona.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |