Katika vitu ambavyo Tanzania inajivunia hasa kwa wana teknolojia na TEHAMA kwa ujumla ni kuwa na kamisheni yao ambayo inaangazia ukuaji, changamoto na kushauri nini cha kuongeza/kuboresha na hapo ndipo kongamano la pili mwaka 2018 linaendeleza gurudumu.
Tangu kufanyika kwa kongamano la kwanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita TeknoKona tulipata bahati ya kuhudhuria na kujifunza mengi tuu kwenye mkutano uliopita na mwaka huu pia si haba tumealikwa tena.
Sasa, katika kila jambo lazima yawepo maandalizi na ili lifanikiwe basi litahitaji umakini mkubwa kuweza kufika malengo na katika kuelekea kongamano la pili litawakutanisha watu mbalimbali (wakereketwa wa teknolojia) kuweza kujadili mambo yanayohusu sekta hiyo.
Kamisheni ya TEHAMA Tanzania imeendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu tukio zima kabla tarehe yenyewe.
Mada ambazo zitazungumzwa kulingana na tarehe husika.
Kwa namna moja au nyingine unaweza ukawa umevutiwa na unataka uhudhurie siku mojwapo kati ya siku tatu (3) za mkutano husika, inawezekana.
Gharama za malipo na jinsi ya kufanya malipo kulingana na siku utakayopenda kuhudhuria.
Iwapo unapenda kujua kuwa Tanzania imetoka wapi/inakwenda wapi basi kongamano ambalo hufanyika kila mwaka si la kukosa na kwa hakika utajifunza mengi.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|