fbpx
Teknolojia, Video

Kucheza magemu hakujalishi umri wala jinsia

kucheza-hakujalishi-umri-wala-jinsia

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Wakati akili imechoka na unahitaji kuipumzisha wakati mwingine unaweza ukaamua kucheza gemu fulani za picha jongefu au kupitia kifaa fulani ukiwa umekaa sehemu badala ya kulala.

Wapo wanaoamini kuwa michezo ya kujifurahisha mathalani ile ya kucheza kupitia televisheni ni kwa ajili ya rika fulani lakini kwa nchi nyingi zilizoendelea si kitu cha ajabu kumuona baba/mama akijumuika na mwanae kucheza gemu na wakafurahi pamoja.

Hata mimi naamini kuwa “Kuchea magemu hakujalishi umri wala jinsia ya mtu” isipokuwa mtu akicheza na kufikia kiwango cha kupata uraibu hapo ndio inakuwa tatizo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika moja la mambo ya takwimu umeonyesha waziwazi rika na asilimia ya watu ambao wanacheza magemu mpaka umri waliofikia na jinsia ya kike hhawapo mbali kabisa na suala hilo.

umri wala jinsia
Rika tofauti tofauti wake kwa waume bado wanajifurahisha kupitia magemu; wastani wa wanawake wenye uri wa miaka 37 na wanaume wenye miaka 33 wanacheza michezo hiyo.

Sasa wewe uliyekuwa unaamini umeshapitwa na wakati kukaa chini na kucheza gemu ondoa fikra hiyo potofu na furahia kitu hicho ambacho ulikuwa unafanya huko nyuma kwani umri wala jinsia si kitu.

Chanzo: Statista

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  M-Safiri; App inayokuwezesha kupata tiketi bila kupanga foleni
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|