fbpx

Tengeneza chanzo cha umeme wa kuchaji simu kwa kutumia viwembe

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Teknolojia zipo nyingi na ukuaji wake unazidi kukua kila siku. Njia mbalimbali za kuweza kuchaji simu zimeweza kugundulika na kutumika hivyo kuendelea kurahisisha/kuboresha mbinu hizo.

Unaweza kushangaa kusikia kitu kama hiki na pengine hukuwahi kufikiria kitu kama wembe unaweza kutumika kuwezesha simu kuweza kujaa chaji tena kwa haraka tu. Basi sisi kama wadau wa teknolojia tumeona kuwa inawezekana na hata wewe unaweza ukatengeneza chaji ya aina hiyo.

INAYOHUSIANA  Kompyuta: Ubora uleule lakini faili ni dogo

Maujanja ya kutumia viwembe kuwezesha kuchaji simu.

Kuna wakati unaweza ukawa mahali na usiwe na uwezo wa kuchaji simu yako na hivyo kukosekana hewani mpaka ule muda ambao utaweza kupata sehemu na ukweka simu ipate chaji. Hapa sasa ndio unaweza kufikiria ni kheri ungekuwa unafahamu njia mbadala wa kuchaji simu iwapo hauna nyezo zilizozoeleka.

Vifaa unavyohitaji kuwa navyo.

a) Viwembe vinne au zaidi, asidi ya Sulphuric ambayo haijachanganywa na maji, vipande vidogo vya boksi, gundi ngumu (solo tape), waya wa chaji ( waya wa USB), karatasi laini za rangi ya fedha, simu janja.

kuchaji simu kwa kutumia viwembe

Kuchaji simu kwa kutumia viwembe : Vitu vinavyohitajika kuweza kuchaji simu kwa kutumia viwembe.

Kujua jinsi ya kuunganisha kila kitu mpaka kuweza kuchaji simu tazama video hii.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kutatua tatizo la "Download pending" kwenye Playstore. #Maujanja

Uwezo wa kuchaji simu kwa haraka au polepole kutategemeana na idadi ya viwembe ambavyo utatumia kutengeneza chaji na chaji hii itakusaidia kukuwezesha kurudi hewani angalau kwa muda mpaka pale utakapokuwa na uwezo wa kuweka simu ipate chaji kisawasawa.

Vyanzo: Info Retweet, Youtube

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.