fbpx

Maujanja, Video, YouTube

Kuangalia Video ya YouTube kupitia VLC kwenye Kompyuta

kuangalia-video-ya-youtube-kupitia-vlc-kwenye-kompyuta

Sambaza

Je kwa sababu yeyote unataka kuendelea kufanya kazi zako kwenye kompyuta na huku ukiangalia video flani, hasa ndefu, kutoka YouTube? Basi kwa kuangalia video ya YouTube kupitia VLC kwenye kompyuta itakurahisishia jambo hilo.

Je kuna faida gani kufanya hivi?

Faida zipo mbili;

  • Utaweza kuangalia video ikiwa juu ya programu zingine zote, na hivyo kukuwezesha kutopitwa na kile unachoangalia. Unaweza hili kwa kubofya View, kisha Always on Top
  • Unaweza pia kudownload video unayoitazama, soma – Shusha Video za YouTube kwa kutumia VLC
INAYOHUSIANA  Litunze Jokofu (fridge) lako kwa Kufanya Haya

Kuangalia video ya YouTube kupitia VLC kwenye kompyuta fuata hatua hizi;

video ya youtube kupitia vlc

  1. Hakikisha una programu ya VLC Media Player kwenye kompyuta yako
  2. Ukifungua VLC, kwenye Menu bofya ‘Media‘, kisha ‘Open Network Stream‘, katika eneo la ‘Network‘ utaona sehemu ya kuweka URL/Anuani ya mtandao.
  3. Kwenye kivinjari chako, nenda kwenye video ya YouTube unayotaka kuiangalia. Bofya kama unataka kuitazama kisha nenda eneo la anuani ya mtandao (url). Chagua yote na bofya ‘Copy’, kisha rudi kwenye VLC na ‘Paste’ url ile kwenye eneo la ‘please enter a network URL‘.
  4. Kisha bofya ‘Play’ au Enter. Video itacheza.
INAYOHUSIANA  Njia rahisi ya kujua sifa ya Kompyuta yako (uwezo wake)

Kumbuka VLC yenyewe itaweza kukuchagulia ubora wa video kulingana na kasi ya huduma yako ya intaneti.

Kufahamu mengi mengine kuhusu YouTube kwenye Teknokona basi tembelea Teknokona/YouTube, kuhusu VLC bofya Teknokona/VLC.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |