Tume ya TEHAMA nchini imeandaa kongamano litakalowahusisha wadau mbalimbali wa teknolojia ya habari na mawasiliano itakayofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 26 na 27 mwezi huu.
ICT (Information Communication and Technology) kwa Kiswahili TEHAMA ni sekta inayokua kwa kasi sana kwa sasa na inayoweza kusaidia ukuaji wa sekta zingine mbalimbali za uchumi.
Kongamano hilo lililobeba jina la kimombo – ANNUAL ICT PROFESSIONALS CONFERENCE, 2017 litawaleta kwa pamoja wadau mbalimbali waliokatika sekta hiyo hii ikiwa ni pamoja na;
- Maafisa wa juu wa serikali,
- Mabingwa wa teknolojia za TEHEMA kutoka mashirika mbalimbali,
- Wawikilishi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali, wafadhili mbalimbali pamoja na makampuni ya kimataifa na ya nchini
- Wasomi
- Maafisa wa TEHEMA kutoka serikalini na sekta binafsi.

Ajenda kuu katika kongamano hilo ni pamoja na kuhimarisha mahusiana kati ya watalaam wa TEHAMA nchini Tanzania na wadau wengine wa TEHAMA nje ya Tanzania kwa lengo la kuifanya Tanzania kuzidi kuimarika katika sekta ya TEHAMA.
- Kutoa mchango wa kimawazo utakaowezesha watu wenye fani ya TEHAMA kuweza kukuza vipato vyao na hatimae kukuza biashara zao. Wadau wenye uzoefu mkubwa kwenye TEHAMA watahusika kumfanya yule anayejishughulisha na masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutokata tamaa.
- Ufafanuzi mpana kuhusu makosa ya kwenye mtandao itakuwa ni moja ya mada katika kongamano hilo ambao maelezo ya kina yatatolewa kuhusu namna gani mdau/mtaalam wa masuala ya TEHAMA anaweza akaepuka na hatari ya kutumia vibaya mitandao ya kijamii, simu, n.k na hivyo kujikuta daima anaepukana na makosa ya matumizi mabaya ya teknolojia.
- Matumizi ya programu tumishi, intaneti, namna ya kuboresha biashara kwa njia ya tehama ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, barua pepe na njia nyinginezo ni masuala yatakayojadiliwa kwenye kongamano hilo.
Matarajio ni kwamba kwa wale watakaohudhuria kongamano hilo ni kwamba mtu atatoka pale na mawazo mapana na mbinu mbalimbali zitazomuwezesha kuwa mmoja ya watu walobobea kwenye suala zima la TEHAMA.
Pia kwa wataalamu mbalimbali itakuwa ni nafasi nzuri ya kuweza kutoa ushauri kuhusu teknolojia ambazo mashirika ya kiserikali yanaweza nufaika nazo.
Kongamano hilo litakuwa la siku mbili (Okt. 26-27) litakalofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwl. J. K Nyerere na ili mtu kuweza kuhudhuria atalipa ada ya Tsh. 200,000/= (kabla ya siku kongamano) na Tsh. 300,000/= (siku ya kongamano).
Kwa taarifa za undani zaidi tembelea tovuti – ictc.go.tz na ict.go.tz
*TeknoKona tunayofuraha kuwa moja kati ya wadau wa kongamano hili.