fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Kompyuta Teknolojia Windows 11

Kompyuta yenye sifa zipi inafaa kuwekwa Windows 11?

Kompyuta yenye sifa zipi inafaa kuwekwa Windows 11?

Spread the love

Matumizi ya kompyuta kwa wengine ni muhimu sana ili kuwezesha kukamilika kwa kazi zao ambapo kifaa hicho kinarahisisha mambo na kuokoa vitu vingi ikiwemo muda. Je, unafahamu kuwa sasa tumefikia kwenye Windows 11?

Binafsi nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa kompyuta na hata kupata taaluma ya masuala ya vitu hivyo kwa muda mrefu nimekuwa mwepesi sana kutoa ushauri wa kitaalamu ana kwa ana au hata kwa njia ya makala kupitia hapa TeknoKona ambapo tumeshaandika makala kadha wa kadha zinazohusisha elimu kwenye maeneo mbalimbali ya kompyuta.

Tangu zifahamike taarifa kuhusiana na ujio wa Windows 11 watu wengi duniani kote wamekuwa na shauku ya kutaka kujaribu toleo hilo la programu endeshi kwenye kompyuta zao na hata wengine wakiwa wameshaiweka kwenye vifaaa vya kidijiti ingawa haijatoka rasmi lakini wengi wakijiuliza sifa gani ambazo kompyuta inafaa kuwa nazo ili programu endeshi iweze kufanya kazi vyema?

Jibu la swali nililouliza ni sawa kwa karibu sana na pale ambapo mtu huniuliza “Kompyuta gani ni nzuri?” Mara nyingi nikijibu swali hili huwa naangalia na teknolojia ya leo imefikia wapi/inahitaji kompyuta za uwezo gani? Nafurahi majibu yangu ambayo nimekuwa nikiwajibu watu yanaendana kwa karibu sana na sifa ambayo kompyuta inatakiuwa kuwa nazo ili Windows 11 ifanye kazi vyema.

>Mosi ni kasi ya kipuri mama. Inaelezwa ni vyema kompyuta ikawa na kasi ya angalau 1GHz au zaidi ili Windows 11 ifanye kazi murua kabisa. Pili, programu endeshi iwe ya toleo la 64bit au “System on a Chip” (SoC) na si 32bit na kimsingi programu nyingi wezeshi zinatoka kutumika kwenye programu endeshi ya 64bit.

>Tatu, nemori ambayo kwa upande ile ya muda kwa maana ya RAM basi iwe angalau ina ukubwa 4GB. Upande wa memori ya kudumu (HDD/SDD) ianzie GB 64 kwenda juu. Nne, kompyuta husika lazima iwe inatumia “Trusted Platform Module” (TPM) ambayo inalenga usalama wa kompyuta nzima; kwaa lugha rahisi kompyuta lazima iwe na uwezo wa kuweka ulinzi kwa kufunga/kufungua ndani ya BitLocker.

>Tano, mashine yenyewe iwe na uwezo wa kuwasha/kuzima katika hali ya kiusalama programu endeshi husika. Vilevile, kipuri mama upande wa picha inatakiwa kuwa kufanya kazi na DirectX 12 au ya juu zaidi sambamba na kiwezeshi (driver)-WDDM 2.0. Sita, ubora wa kioo unatakiwa ni kuanzia 720px au zaidi. Halikadhalika, urefu wa kioo uwe ni kuanzia inchi 9 kwenda juu.

Windows 11

Muonekano wa Windows 11 ambayo kimsingi inahitaji komyuta yenye uwezo wa kati kuweza kufanya kazi vizuri.

Mwisho lakini si kwa umuhimu ni lazima kompyuta husika iwe na uwezo wa kuunganisha intaneti lakini pia akaunti mbalimbali za Microsoft kuweza kufanya kazi.

“Kila mwamba ngoma huvutia kwake” hivyo usishangae ulazima akaunti za Microsoft kwani zitahitajika kuweka mambo wakati wa kuiweka ndani ya kompyuta.

Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] tumeshaandika makala kuhususiana na sifa gani kompyuta inatakiwa kuwa nazo ili kuwa na uwezo wa kukubali Windows 11 hata hivyo wapo wale ambao wataishusha na kuiweka kwenye vifaa vyao […]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania