Unakumbuka siku chache zilizopita tuliandika habari kuhusu kivinjari cha UC Browser kuondolewa katika soko la apps la Google Play store?Lakini leo tunakujuza kwamba rasmi kivinjari hicho kimerudishwa katika soko hilo kama ilivyokuwa awali.
UC Browser iliondolewa katika soko la Google Play kwa taarifa zilizoelezwa ingawa hazijathibitishwa kwamba imekuwa ikichukua data za watumiaji wake na kuzilepeka China bila ya idhini ama kuongeza idadi ya upakuaji (download) wake katika njia za udanganyifu. Kufahamu zaidi kuhusu kwanini UC Browser iliondolewa kwenye Play Store BOFYA HAPA!
Mbali na sababu hizo hakuna aliyewahi kuthibitisha kwanini UC Browser iliondolewa katika soko la Apps la Google Play Store. Kuondolewa kwa UC Browser katika soko la Google Play kuliathiri watu wengi ambao wamekuwa wakitumia App hiyo. UC Browser imekuwa ikiwavutia wengi kwa ubora wake na utumiaji mdogo wa Data.