Je huwa unakuwa mpweke sana? – Iwe unasafiri au upo tu sehemu kama nyumbani, Toyota waja na roboti mdogo kwa ajili ya kukuondolea upweke. Anaitwa Kirobo.

Roboti mwenye ukubwa mdogo, urefu wa inchi 4 tuu, anaweza zungumza na wewe na ata kusoma muonekano wa sura yako na hivyo kuweza kufahamu kama umekasirika au ni mwenye furaha na hivyo kutambua jinsi ya kuwasiliana na wewe.
Kupitia video fupi inayomtangaza roboti huyo iliyotolewa na Toyota inaonesha roboti huyo akifurahia pale dada anayeongea akitabasamu – na anauliza kuna jambo jipya la kufurahisha. Uso ukiwa na uzuni pia anauliza akitaka kufahamu tatizo ni nini.
Watu wa Japan wanapenda sana utumiaji wa maroboti na ni nchi iliyo mbele sana katika utengenezaji wa teknolojia hizo.
Kwa sasa wamesema roboti huyo, Kirobo, ataanza kupatikana nchini Japan mwakani ila bado hawajatoa taarifa za upatikanaji wa roboti huyo nje ya Japan na katika lugha zingine.
Bei je?
Bei ya roboti hiyo itakuwa takribani dola 400 za Kimarekani (Kwenye Tsh 1,000,000/= hivi), na atauzwa kupitia mawakala wa magari ya Toyota.