Watumiaji wa WhatsApp duniani kote wanapokea masasisho mbalimbali ambayo programu tumishi husika inafanyiwa kwa lengo la kuifanya iwe bora zaidi. “Focus Mode” ni kipengele kipya kilichowekwa huko.
Katika siku za karibuni WhatsApp imekuwa inaboreshwa mathalani uwezo wa kugandisha na kisha kuendelea kurekodi jumbe ya sauti ikichukua nafasi ya kitufe cha kuacha (stop). Baada ya hilo sasa kuna jingine jipya ambalo limeonekana kuanza kwa watumiaji wa WhatsApp Marekani wenye simu za iPhone zinazotumia iOS 15.
Hivi sasa kuna kipengele kipya kwenye WhatsApp kinachoitwa “Focus Mode” ambacho kinamuwezesha mtumiaji kuchagua taarifa fupi ambazo angependa kuziona wakati jumbe zinapoingia kwenye simu janja. Pia, kipengele hiki kinawezesha kuonyesha picha ya mtu aliyoweka kwenye akaunti yake.

Kipengele hiki kinatazamiwa kuanza kupatikana kwa watu wote ndani ya wiki chache zijazo na ni muhimu kwa watu kuwa na toleo la karibuni kabisa la iOS. Hakuna neno lilitoka kuhusu kipengele hicho kwenye Android lakini tutawahabarisha mara tu itakapofahamika.
Lakini kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia kwani ndio kazi yetu na kuwa na wasomaji wengi kwenye tovuti yetu ndio furaha yetu.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
One Comment