Kipaumbele cha soko letu ni Afrika #Tecno

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Bw. Andy Yan, Makamu Rais wa kampuni ya Transsion Holdings inayomiliki kampuni Tecno Mobile amesema soko la Afrika ndio kipaumbele cha kampuni yake kabla ya kufikia soko la ulimwenguni kote.

Takribani miaka kumi na miwili (12) iliyopita kampuni ya Transsion ilianza uwekezaji Afrika na siku zote wamekuwa wakiangalia masoko ya Afrika ya kati na Magharibi kwa namna ya pekee kutokana na fursa kubwa iliyoko huko.

INAYOHUSIANA  Rasmi: Uzinduzi wa iPhone 8 kufanyika Septemba 12 mwaka huu

Nchi za Ghana na Ivory Coast ni muhimu sana kwa soko la simu za Tecno ambapo kwa nchi ya Nigeria tayari soko kwa upande wa Tecno limeonekana kuwa kubwa na imara katika nchi yenye watu milioni 200.

Kipaumbele cha soko

Bw. Andy Yan, Makamu Rais wa Transsion Holdings inayomiliki Tecno Mobile.

Bidhaa zao (Tecno) zimeendelea kununuliwa sana Afrika kwa watu wa matabaka tofauti tofauti kwa kuwa bei zao zimekuwa rafiki hata kwa watu wa kipato cha chini. Kadhalika, kuongezeka kwa mapato na kushika soko la simu kwa baadhi ya nchi kadhaa Afrika imetokana na Tecno kuingia ushirikiano na kampuni kadhaa za mawasiliano katika nchi wazouza simu zao.

Kipaumbele cha soko

Mpaka sasa Transsion Holdings ina maduka katika nchi 13 kutoka bara la Afrika.

Aidha, Tecno wameendelea kuimarisha soko lake kwa baadhi ya nchi katika bara la Afrika ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.