fbpx

Kati Ya Pin Na Pattern, Kipi Bora? #Android #Usalama

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Ufunguaji wa simu wakati ikiwa imelokiwa ulikua ni rahisi sana hapo mwanzo, lakini kumbuka kuwa ilikua ni rahisi vile vile kuweza kuibiwa taarifa zako kwani mtu angeweza kufungua kifaa chako kwa urahisi.

Teknolojia imekua na vilevile simu zetu zinahifadhi karibia kila kitu chetu mpaka vile vya siri. Je, ni njia gani ya msingi ya kuitumia kati ya ‘Pin au Pattern’ ili kujihakikishia usalama wa hali ya juu?

Simu nyingi za zamani kama vile Nokia na zingine ilikua inakuladhimu kubonyeza vitufe viwili kwa haraka ili kuweza kufungua simu hiyo (menyu na nyota). Lakini vipi kwa simu za kileo (simu janja), hapa ndipo habari nyingine inapokuja.

Pin na Pattern

Pin na Pattern: Jinsi Ya Kufungua Loki Ya Android Kwa Kutumia Pattern Vs Kutumia Pin

iOS Vs. Android.

Apple kwa mara ya kwanza walianzia teknolojia ya ‘Slide to unlock’ ambayo Steve Jobs mwenyewe alisema ni njia rahisi ya kuzuia simu kujipiga au kujibonyeza yenyewe pindi ikiwa mfukoni mwa mtu. Vilevile Apple walikua na jinsi ambavyo mtumiaji wa vifaa vyake  anaweza kuweka loki (maarufu kama passcode) kwa kutumia pin nne (Sasa anaweza hadi kuweka pin sita).

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!

Android

Tukija kwa Android njia maarufu ya kuweza kutoa ulinzi (lock) katika simu ni kwa kutumia ‘Pattern’ ambapo njia hii inasemekana sio ya kuisalama sana kama vile watu wanavyofikiria. Yaani kati ya kutumia Pin na Pattern ni bora mtumiaji wa Android atumia Pin ili kujihakikishia usalama wa hali ya juu.

Wataalamu wa ulinzi na usalama wa Marekani, Naval Academy wamefanya utafiti ambao umebainisha hilo pamoja na kushirikiana na chuo kikuu cha  Maryland Baltimore County. Katika utafiti huo iligundulika kuwa ni rahisi sana kushika Pattern za simu ya mtu pindi akiwa anafungua simu yake kuliko yule ambae anatumia Pin.

Kumbuaka katika Pattern ni rahisi sana kuweza kufuatilia njia ambayo mtu anapita katika kukamilisha Pattern hiyo lakini Pin ni ngumu kidogo kwani anarukaruka tuu.

KITU CHA KUFANYA

INAYOHUSIANA  WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

Kama ni mtumiaji wa Android, fanya juu chini uachana na kutumia ‘Pattern’ na uhamie katika ‘Pin’ tena utumie zile zenye tarakimu sita kwa usalama zaidi. Lakini vilevile labda dunia inapokwenda sasa hivi kutakua hakuna haja tena ya kuwa na ‘Pattern’, kwa sasa simu zinatolewa loki kwa kutumia alama za vidole vile vile hata kwa uso (iPhone X).

Nipe mawazo yako sehemu ya comment hapo chini. Hivi ni mara ngapi umebadilisha ‘Pattern’ ya simu yako kisa tu mtu kaiona na ulikua hutaki aijue?

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.