fbpx

Kaspersky Lab washinda zabuni Brazil kuhudumia jeshi la nchi hiyo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kampuni ya Kaspersky Lab imeshinda zabuni ya kutoa huduma za usalama wa kimtandao kwa vikosi vya jeshi la nchi ya Brazil.

Kaspersky Lab washinda zabuni Brazil

Kaspersky Lab washinda zabuni Brazil

Baada ya ushindaji mkali wa mchakato wa kutafuta kampuni stahiki ya kufanya kazi hiyo Kaspersky Lab ilipata zabuni hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya dola milioni 2.6.

Dola Milioni 1.4 itakuwa kwa ajili jeshi la Anga pekee, Dola 735,000 kwa Ulinzi wa kimtandao na Dola 512,000 kwa ajili ya jeshi la majini. (Dola moja ya Marekani ni takribani Tsh 2,250/= kwa sasa)

INAYOHUSIANA  Kaspersky yakiri kupakua nyaraka za siri za Marekani

Kaspersky Lab haikutoa maelezo ya programu gani maalum ambazo Vikosi vya Jeshi la Brazili zitatumia au wakati wa kuanza kazi hiyo.

Lakini tangazo rasmi la kampuni hiyo linasema kwamba kompyuta 120,000 zitakuwa na programu mpya ya Antvirus ya Kaspersky.

Wiki iliyopita, Marekani kupitia wizara ya Usalama wa Nchi (DHS) ilitoa maelekezo kwa ofisi zote za serikali kuacha matumizi ya programu ya Kaspersky kwa sababu ya wasiwasi na uhusiano wa kampuni na nchi ya Urusi.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.